Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - (Uwekezaji) Mhe. Geoffrey I. Mwambe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu. I. Kazi  wameshiriki katika kongamano la Taasisi za Uwekezaji Afrika lililofanyika Sharm El Sheikh nchini Misri. Kongamano hilo linaongozwa na Mhe. Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu wa Misri kuanzia tarehe 11 hadi 14 June, 2021.Mhe. Waziri wa Uwekezaji Mwambe na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt Maduhu wamefanya mikutano mingine na wawekezaji mbalimbali waliowekeza nchini Tanzania na ambao walionyesha nia ya kuwekeza nchi kutokana na sera nzuri na mazingira ya uwekezaji yaliyopo nchini. Katika mikutano hiyo Mhe. Mwambe aliweza kukutana na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya El Sewedy Electric, Eng. Ahmed El-Sewedy ambae ni muwekezaji wa Tanzania kampuni hii inaendelea kufanya kazi nchini Tanzania. Pia wanaendelea na mipango ya kupanua zaidi uwekezaji wao nchini hasa katika eneo la viwanda na maeneo maalum ya viwanda.Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dkt. Maduhu I. Kazi wakifanya mazungumzo na Eng. Ahmed El Sayed Ahmed, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Giza cable industries ya nchini Misri ambayo ina mpango wa kuwekeza nchini Tanzania kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 50 katika kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme (electrical cable manufacturing), kulia ni Bw. Revocatus A. Rasheli, Mkurugenzi Huduma kwa Wawekezaji. Aidha, Dkt. Maduhu amemkabidhi Eng. Ahmed El Sayed Ahmed, nyaraka zinazoonyesha namna ya kuwekeza nchini na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo.Mhe. Geoffrey I. Mwambe, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, akiwa kwenye majadiliano ya pamoja (panel discussion) kwenye kongamano la taasisi za uwekezaji za nchi za Afrika (IPAs Africa Forum) ambapo Mhe. Waziri amezungumza mada kuhusu (Africa’s Pursuit for a Bigger Role in Global Market). Katika kongamano hilo, ni nchi mbili tu za Afrika ikiwemo Tanzania ndio imepata mwaliko wa Mawaziri wanaohusika na uwekezaji kushiriki kama wageni maalum kwenye kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...