Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameitaka Bodi ya Maziwa Tanzania (BMT) kuweka mikakati thabiti ya upatikanaji wa keni za kubebea maziwa (Milkcans) ili kusaidia ukusanyaji wa maziwa hapa nchini.Hayo ameyasema leo (12.6.2021) jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Viongozi pamoja na wakuu wa Idara kutoka BMT pamoja na Bodi ya Nyama Tanzania.

 Mhe. Ulega alisema hivi karibuni, katika Bajeti kuu ya serikali yapo mapendekezo ya kuondoka kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye milk cans zinazotambulika kwa HS code 73.10.00 na 7310.29.90 kwa lengo la kuweka unafuu kwenye bidhaa hizi ili hayo yawezeshe kurasimisha tasnia ya maziwa na kuongeza fursa za biashara kwa wazalishaji wa maziwa hapa nchini.

 Mhe. Ulega ameitaka Bodi ya Maziwa kushirikiana na viwanda vya maziwa, TAMISEMI pamoja na wabia wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa hamasa kubwa inatolewa ili kuongeza uzalishaji na usambazaji wa milk cans kwa wingi hapa nchini baada ya kuwepo kwa unafuu unaopendekezwa.

 "Bodi ya Maziwa tunataka mshirikiane na viwanda vikubwa, vya kati, na vidogo katika kuhakikisha milkcans zinaenda kwa wingi kwa wadau na hasa ziwafikie akina mama na vijana katika Halmashauri zetu nchini" alisema. Aliongeza kuwa BMT wawashawishi Wakurugenzi wa Halmashauri (DEDs) na kwa kushirikiana na wataalam wa TAMISEMI wakiwemo (Maafisa Mifugo, Maafisa Ushirika, na Maafisa Maendeleo ya Jamii) kuhakikisha asilimia 10% ya mapato ya mifugo inatolewa kwa akina mama na vijana kama mikopo kwa ajili ya tasnia ya maziwa na fedha hizo zisaidie kununua cans na ukusanyaji wa maziwa.

 Nae Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dkt. George Msalya amesemakwa takwimuzilizopo ni takribani asilimia 3 tu ya maziwa yanayozalishwa nchini yanafika katika viwandani kwa ajili ya kuchakatwa na hivyo, maziwa yanayoingia katika mfumoulio rasmi ni kidogo.

 Dkt Msalya amesema hali hii inatokananakukosekana kwa mifumo mizuri na ukusanyaji wa maziwa na gharama kubwa ya ununuzi wa vifaa vya kukusanyia maziwa zikiwemo milk cans. Aliongeza kuwa kwanafuuinayotolewa, Bodi inajipanga cans zipatikane kwa wingi na kuwafikia akina mama na vijana kama alivyoagiza Mhe. Naibu Waziri. Ameahidi kushughulikia swala la mfumoili Taarifa za hali Halisi ya maziwa (uzalishaji), ukusanyaji, na vituo vya kukusanya maziwa ziapatikane kwa urahisi.

 Dkt. Msalya amesema Bodi ya Maziwa itashirikianana TAMISEMI hasa Wakurugenzi na Wadau mbalimbali wa tasnia ya maziwa kuhakikisha kuwa maziwa yanakuwa biashara yenye tija kupitia punguzo kwenye milk cans na mikakati ya Wizara zikiwemo “Kopa ng’ombe lipa ng’ombe”na “Kopa mbuzi lipa mbuzi”

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akizungumza na watumishi wa Bodi ya Maziwa Tanzania (BMT) juu ya kwenda katika Halmashairi na vikundi vya Vijana na wakina Mama wanaojihusisha na maziwa kuhamsisha ukusanyaji wa maziwa ili kuongeza mnyororo wa thamani ya maziwa,mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.kushoto Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dkt.George Msalya  kulia Kaimu Meneja Bodi ya Nyama,Johan Chassama.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Watumishi wa  Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakimsisikiliza  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kushoto) akiteta jambo na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dkt.George Msalya 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Slaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...