Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAFANYAKAZI watatu wa Taasisi ya fedha ya Letshego maarufu kama Faidika Limited, wamefikishwa katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la la wizi wa sh milioni 700.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Faraja Ngukah mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Elisha Tengeni , Donald Kwaya na Elisha Mboka.

Akisoma shitaka hilo, wakili Ngukah aludao alidai kati ya Januari mwaka 2016 hadi Septemba mwaka 2017  washitakiwa waliiba sh milioni 700 mali ya Kampuni ya Letshego Tanzania Limited  maarufu kama Faidika fedha ambazo zilifika kwao kutokana na nafasi zao za uwajili.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao wasilisha mahakamani fedha taslim au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 350.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Juni 30 mwala huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wote wamepelekwa maabusu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...