TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) inaendesha mafunzo ya ujaribishaji wa miongozo ya elimu ya stadi za Maisha kwa walimu  wa shule za Msingi  na Sekondari nchini.

Akifungua mafunzo hayo katika wilaya ya Temeke ,Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala (TET) Bi.Fika Mwakabungu amesema kuwa ,walimu  1696 katika halmashauri 13 nchini watapatiwa mafunzo hayo na kisha wataweza kuwafundisha wenzao ili wakatoe uelewa wa stadi za maisha.

"Karne hii  ya 21 wanafunzi wanapaswa kuandaliwa mapema kwani wanakutana na mambo mengi hivyo tunapowaandaa mapema kujua masuala mbali mbali wataweza kuepukana na changamoto" alisema Bi Fika.

Mafunzo hayo ya stadi za maisha yanahusisha masuala ya afya,afya ya uzazi,Vvu na ukimwi na jinsia na namna ya kuondokana na ukatili  wa kijinsia.

Kwa upande  wake,mwezeshaji wa mafunzo hayo ,Bi.Amina Tou ameeleza kuwa,wana imani walimu wanaohudhuria mafunzo hayo wataweza kuwaelimisha wengine katika shule zao ambapo pia watahakikisha kwamba wanafunzi watakaopewa elimu hiyo iwasaidie.

Mafunzo hayo  yameanza kufanyika leo katika halmashauri 13 ambazo ni; Ilala, Temeke, Ngorongoro, Ifakara, Kasulu, Kisarawe, Kibondo, Ulanga ,Morogoro mjini,Malinyi,Sengerema,Bagamoyo na Mlimba.

Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala wa Taasisi ya Elimu Tanzania  (TET), Bi.Fika Mwakabungu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Ujaribishaji wa miongozo ya elimu ya stadi za Maisha kwa Walimu  wa shule za Msingi  na Sekondari nchin, yaliyofanyika Wilaya ya Temeke na Halmashauri zingine 12 nchi nzima.


Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...