Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Watanzania wameaswa kutumia nafasi zao katika jamii ili kuendelea kuitangaza nchi katika nyanya mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii na uwekezaji.

Hayo yamesemwa na Afisa Polisi kutoka Nchini Tanzania anaehudumu Umoja wa Mataifa katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo Ally Babu wakati wa tafrija ya Chakula cha Usiku kwa maafisa hao.

Babu  ameendelea kuitangaza nchi katika utalii na uwekezaji na kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi kutumia fursa hiyo kuitangaza nchi ili kuwavutia wawekezaji na watalii kuja kuwekeza kwa wingi.

Katika tafrija hiyo, Babu amewahakikishia wawekezaji uwepo wa usalama, hali ya hewa nzuri na sheria bora za uwekezaji zinazomlinda kwa asilimia kubwa na ushirikiano mzuri kutoka kwa watanzania.

Aidha amewaomba wafanyakazi wenzake kutengeneza umoja na mshikamano wa kidunia na kuacha michoro ya mipaka katika ramani.

 Babu ambae pia ni mwanasheria kitaaluma amekuwa moja ya maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Congo anayetumia nafasi yake kuweza kuutangaza utalii wa Tanzania na kufundisha lugha ya Kiswahili kwa maafisa kutoka nchi mbalimbali.

Pia katika hafla hiyo amepongezwa kwa utendaji wake wa kazi uliotambulika ndani na nje ya Umoja wa mataifa nchini Congo.

Afisa Polisi kutoka Tanzania anayehudumia Umoja wa Mataifa Katika nchi ya Kidemokrasia Congo Ally Babu (kushoto) akipokea tuzo ya utendaji bora wa kazi ndani na nje ya nchi hiyo kutoka kwa moja ya wawakilishi wakati wa hafla ya Chakula cha Jioni kwa maafisa hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...