Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma,  Nyakimura Muhoji amewataka Waajiri, Mamlaka za Ajira, Mamlaka za Nidhamu pamoja na watumishi wote wa Umma kuhakikisha wakati wote wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maelekezo halali yanayotolewa na Serikali.

  Muhoji amesema hayo katika taarifa aliyoitoa kwa umma kuwa Tume ya Utumishi wa Umma itasikiliza watumishi wa umma na wadau wake wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoanza kesho Jumatano tarehe 16 hadi 23 Juni, 2021.

“Tume katika maadhimisho ya mwaka huu  imeandaa utaratibu ambapo Maafisa wa Tume watapokea na kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi wa umma kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi. Kuanzia Jumatano tarehe 16 hadi 18 Juni, 2021 Maafisa wa Tume watakuwa wilayani Kisarawe, mkoani Pwani na tarehe 21-23 Juni, 2021 watakutana na wadau katika Ofisi ya Tume iliyopo Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam” amesema Bwana Muhoji.

 Muhoji ametoa wito kwa watumishi wa umma na wadau waliopo Kisarawe na Dar es Salaam kufika kwa tarehe hizi mahsusi zilizopangwa ili waweze  kuhudumiwa na Maofisa wa Tume kuweza kuzitafutia ufumbuzi  changamoto zinazowakabili kiutendaji.

“Watumishi wa umma na wananchi watakaoshindwa kufika amesema wanaweza kuwasilisha kero na malalamiko yao kwa kutuma barua pepe kwa anuani ya secretary@psc.go.tz au kupiga simu namba 0738 166 703” amesema.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2021 ni: “Kuheshimu tofauti ya nyenzo za kuimarisha misingi ya utawala wa umma ulio adilifu.”

Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kuhakikisha kuwa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma inasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...