Na Mwandishi Wetu,Tanga

KATIBU  wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka usiku huu 12,  Juni 2021 amekutana na kuzungumza na Wazee wa mbali mbali wa  Wilaya ya Pangani katika ukumbi wa Halmashauri ya Pangani

Wazee wamepongeza utendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali huku wamemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kulipa fidia kwa Wananchi ili kupisha ujenzi wa barabara ya Tanga, Pangani, Saadani - Bagamoyo pamoja na kuwapatia 1.80 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

"Tunamuombea kwa Mwenyezimungu sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan kadri ya Siku zikienda imani inaongezeka kwake  anatufariji na tunauona mwanga mkubwa kwa  Tanzania kupiga hatua kubwa za maendeleo,"amesema  Mzee Simai Hija wa Pangani Mashariki.

Wilaya ya Pangani ina wazee 6,691 waliopatiwa vitambulisho 3859 walemavu 689 utaratibu wa kuwatambua wote unaendelea kukamilishwa.

Katika hatua nyingine, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Shaka amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kujituma zaidi katika ujenzi wa Chama pamoja na kuisimamia Serikali katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025 katika ngazi zao.
 
Ameyasema hayo leo alipokutana na wanachama wa CCM wa Shina namba 3,15 na 20 katika Kata za Madanga, Mwera na Pangani Magharibi Wilayani Pangani Mkoani Tanga.
 
“Ndugu zangu tumekuja kutoka Taifani na kukutana na wanachama wetu katika ngazi za chini kabisa ya Shina kwa sababu Katiba ya CCM imebainisha kuwa Shina ndio msingi na moyo unaoleta uhai wa Chama ni mashina ndio yenye kuwatambua wanachama na hali zao na hivyo kuelewa uhai na nguvu ya chama. Hivyo tumeona tujiimarishe zaidi katika ngazi ya Mashina ili tuwe na chama imara zaidi."
 
Amesema kuwa Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ndio wenye wajibu wa msingi kabisa wa  kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao kwa niaba ya Chama kwani kufanya hivyo ndipo Chama kinapata uhalali kwa wananchi.
 
Akiwa katika ziara hiyo katibu wa Itikadi na Uenezi alizungumza kwa Njia ya Simu na Mbunge wa Jimbo la Pangani ambaye pia ni waziri wa maji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Juma Aweso katika utatuzi wa Kero mbalimbali katika jimbo hilo na kupata majawabu kama ilivyostahili.

Katibu Mwenezi anaendelea na ziara yake ya kuimarisha Chama Mashinani katika Mkoa wa Tanga, ambapo baada ya kukamilisha ziara yake leo Wilaya ya Pangani kesho tarehe 13 Juni 2021 ataelekea Wilaya ya Muheza ambapo atatembelea mashina katika Kata mbalimbali Wilayani humo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wazee mbalimbali wilayani Pangani mkoani Tanga.
Sehmu ya wazee wa wilaya ya Pangani mkoani Tanga wakiwa makini kumsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka( hayupo pichani) ambaye amekutana na kufanya nao mazungumzo yaliyohusu masuala mbalimbali yanayohusu wa wazee wilayani humo

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...