WAZIRI wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula akijibu maswali ya wabunge Bungeni Jijini Dodoma
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia NGOs Neema Lugangira akitoa Mchango wake kwenye Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje


WAZIRI wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula amesema kabla ya mwaka huu kuisha Sera ya Nje inayojumuisha Sera ya Diaspora itakuwa tayari na hiyo ni kwa kutambua uhimu wa diaspora katika kuchangia maendeleo na masuala ya diaspora yanapewa kipaumbele.


Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu kuhusu Ushauri aliotoa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia NGOs Neema Lugangira katika Mchango wake kwenye Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje alipoitaka Serikali itunge Sera ya Diaspora ambayi ni Sera hiyo ni muhimu na kwa sababu jambo hilo haliwezi kuendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje pekee kwa sababu linahusu Sekta nyingi.


“Mh Spika ningependa kugusia suala la diaspora hili jambo lilishawai kujadiliwa sana na tulishapiga hatua ambapo diaspora hao mikutano mbalimbali ilifanyika nje ya nchi na walishiriki hata kutoa maoni kwenye katiba mpya ambayo inapendekezwa sasa nimefurahi kwenye Hotuba, Mhe Waziri amewagusia suala la diaspora na hata kwenye mapendezo ya kamati nao wameguaisia suala la diaspora" Alisema

Mbunge Lugangira aliendelea kusema kwamba lile zoezi la ziara nyingi nje ya nchi zilizokusanya maoni ya diaspora na hadi kuwashirikisha diaspora kwenye huo mchakato Katiba mpya inayopendekezwa yalipelekea hayo kuanzishwa kwa Idara ya Diaspora ndani ya Wizara na Mambo ya Nje ambapo kulikuwa na Mkurugenzi kwenye jukumu la kufanya coordination na ufuatiliaji.

Aliendelea kusema kwamba hivi sasa imeonekana kama jambo hilo limerudi nyuma kwa sababu hivi sasa kuna Sheria ambazo zinamzuia Mtanzania anayeishi Nje ya Nchi kumiliki ardhi lakini pia zipo Sheria ambazo zinamnyima haki ya kurithi mali za wazazi wake kwa sababu Sheria zimeweka hicho kizuizi na kwa msingi huo anapendekeza Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi iandae Sera ya Diaspora.

Alisema kwa sababu nchi nyengine wanatumia diaspora kuendeleza uchumi na uwekezaji hivyo Serikali itunge Sera ya Diaspora na Sera hiyo ni muhimu kwa sababu nasi pia Tanzania tutaweza kutumia diaspora kuchangia kukuza uchumi wa nchi yetu ambayo ni nchi yao pia.

“Mh Spika Mbunge mwenzangu ametoa mfano wa India lakini naomba nilitolee ufafanuzi. Nchini India walichofanya wamewapa Wahindi wanaoishi Nje ya India kitu kinachoitwa Pasipoti ya People's of India Origin (PIO) ambayo PIO hiyo inamruhusu mwenye pasipoti ya PIO kuingia India na kutoka muda wowote bila Viza, in mruhusu kuwekeza kwenye hiyo nchi na kufanya kazi kwenye Sekta zote kasoro Sekta ya Ulinzi na Usalama” Alisema Mbunge Neema Lugangira

Alisema pia "Jambo lingine ambao Wahindi wenye Pasipoti ya PIO ambalo hawatakiwi kufanya ni kujishughulisha na masuala ya kisiasa na kupiga kura hivyo mantiki hiyo Mhe Spika napendekeza na sisi kama Tanzania tufike huko na hatuwezi  kwenda huko bila kuwa na Sera ya Diapsora na Sheria ambayo itaelekeza ni namna gani tutatoa fursa kwa diaspora.

“Katika jambo hili naomba tusichanganye mambo mawili ya diaspora na uraia pacha hilo la uraia pacha tumelijadili na limeoneka lina ugumu hivyo lisituchukulie muda lakini la diaspora lipo ndani ya uwezo wetu na hata sasa hivi diaspora wananunua viwanja wanawekeza na wanafanya hivyo kutumia kwa kutumia njia zisizo rasmi kwa kutumia ndugu jamaa na marafiki “Alisisitiza Mbunge Neema Lugangira

Alisema hivyo wanachotakiwa kufanya ni Wizara ya Mambo ya Nje iwe na Sera ya Diaspora ili kuweka suala hilo rasmi na kupitia Sera hiyo Nchi itaweza kujua kuna diaspora wangapi na mchango wao katika ukuaji wa uchumi ni upi.

“Kwa kumalizia naomba Mhe Waziri atapokuja kuhitimisha atuambie na atupe Msimamo wa Serikali wa kuja na Sera ya Diaspora ambayo itawezesha Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi kuchangia kwenye maendeleo ya nchi na kutoa rasimali fedha amboyo tunaihitaji kwenye uwekezaji ”Alisema Mbunge Neema

Awali wakati anaanza Mchango wake Mbunge Neema Lugangira alisema "Nampongeza sana Mhe Rais Samia Suluhu kwa ziara aliyoifanya nchini Kenya ambayo imeleta matokeo makubwa sana katika diplomasia ya uchumi inayohitajika nchini na kama unavyofahamu wiki hii Kenya na Tanzania wamekubaliana kuondoa Tozi za biashara 30 na kuna mchakato wa kuondoka Tozo 34 na hayo ni matokeo ya jitihada kubwa za Mhe Rais lakini pia nimpongeze Mhe Waziri wa Viwanda na Baishara kwa kufanikisha jambo hilo".

Mbunge Neema Lugangira alisisitiza kwamba Mtazamo wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Kenya kwamba sio adui wetu uungwe mkono kwani Kenya ni mshindani mwenzetu, wanatupa changamoto, tusiwaogope kutokana na kwamba tunaweza kushindana nao na kuwakabili.

“Niungane na Wabunge wenzangu ambao wametoa pongeza kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kutengeneza safu mpya kwenye Wizara ya Mambo ya Nje iliyojaa wabobezi kwenye fani ya diplomasia ikiongozwa na Waziri Balozi mwanamama Liberata Mulamula, Naibu Waziri Mbaruku, Katibu Mkuu Balozi Sokoine, Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Rajabu na Chief Protocol Balozi Mndolwa  ambao tunaimani nao kubwa sana na sasa tunaona diplomasia nchini inapaa” Alisema Mbunge Lugangira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...