Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akitoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa aliyemaliza muda wake John Magalle Shibuda mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya katika kikao kilichofanyika kwa siku mbili na kuhitimishwa kwa uchaguzi leo jijini Dodoma. Kushoto ni Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt. Abdulla Sadalla Mabodi.



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda akitoa neno la shukrani mbele ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya leo jijini Dodoma.



Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Dkt. Abdulla Sadalla Mabodi akitoa neno la shukrani mbele ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya leo jijini Dodoma.



Msimamizi wa Uchaguzi wa Viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa na wawakilishi wa wagombea wana nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa wakiwa katika zoezi la kuhesabu kura wakati wa kikao cha Baraza hilo leo tarehe 28 Julai, 2021 jijini Dodoma.Wagombea wa nafasi hiyo walikuwa Ndg. Juma Khatib na John Shibuda wote kutoka Chama cha TADEA Zanzibar na Tanzania Bara mtawalia.



Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Juma Khatibu akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi ulifanyika sambamba na kikao cha Baraza hilo leo tarehe 28 Julai, 2021 jijini Dodoma.



Makamu Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vyama vya Siasa ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Bibi. Christina Mndeme akizungumza mbele wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kupita bila kupingwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi ulifanyika sambamba na kikao cha Baraza hilo leo tarehe 28 Julai, 2021 jijini Dodoma.



Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akimpongeza Makamu Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vyama vya Siasa ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Bibi. Christina Mndeme baada ya kupitishwa bila kupingwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi ulifanyika sambamba na kikao cha Baraza hilo leo tarehe 28 Julai, 2021 jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohammed Ally Ahmed(kushoto) na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza.



Mjumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kakiwakilisha Chama cha ACT –Wazalendo, Juma Duni Haji akitoa nasaha mara baada ya kupatikana kwa viongozi wapya wa Baraza hilo leo jijini Dodoma.



Kutoka kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohammed Ally Ahmed, aliyekkuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ndg. John Shibuda, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Dkt. Abdulla Sadalla Mabodi na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya leo jijini Dodoma. (Picha na ORPP)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...