Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MICHEZO ya Play-Off rasmi imekamilishwa leo kwa timu zilizokuwa zinashiriki Ligi Kuu Soka Tanzania msimu uliopita za Coastal Union ya mkoani Tanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro kubaki kwenye Ligi hiyo baada ya ushindi katika michezo yao iliyopigwa nyumbani na ugenini, michezo iliyopigwa Julai 21 na Julai 24 mwaka huu.

Coastal Union (Wagosi wa Kaya) wamebaki Ligi Kuu baada ya ushindi wa jumla ya mabao 5-3 dhidi ya Pamba FC kutoka mkoani Mwanza, mchezo wa kwanza uliochezwa Mwanza (Julai 21, 2021) Coastal waliambulia sare ya bao 2-2 ugenini kwenye Uwanja wa Nyamagana, mchezo wa mwisho katika dimba la Mkwakwani, Wagosi wa Kaya wameondoka na ushindi wa bao 3-1.

Mabao ya Coastal Union yaliyoibakisha Ligi Kuu yamefungwa na Mshambuliaji, Abdul Hamis (Sopu) aliyefunga mabao mawili huku bao la tatu Golikipa wa Pamba FC akijifunga mwenyewe dakika za lala salama za mchezo huo.

Wanatam tam, Mtibwa Sugar kutoka Morogoro wamebaki Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2 dhidi ya Transit Camp ya Dar es Salaam, katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Uhuru, Mtibwa walipata ushindi wa bao 4-1 ugenini, licha ya ushindi huo Transit Camp walipata ushindi wa bao 1-0 katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.

Kwa matokeo hayo timu hizo zitabaki Ligi Kuu na zitaungana na timu za Simba SC, Yanga SC, Azam FC, Biashara United, KMC FC, Polisi Tanzania, Tanzania Prisons, Dodoma Jiji FC, Namungo FC, Mbeya City, Ruvu Shooting FC na Kagera Sugar na Mbeya Kwanza FC, Geita Gold FC zilizopanda kushiriki msimu ujao.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...