Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza na Wakuu wa Ukaguzi wa Ndani na Wahasibu Wakuu wa Wizara na taasisi zake (hawapo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa ripoti ya CAG kilichofanyika Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Ukaguzi wa Ndani na Wahasibu Wakuu wa Wizara na taasisi zake (hawapo pichani) kuhusu uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa ripoti ya CAG kilichofanyika Dodoma
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, CPA. Joyce Christopher akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Wakuu wa Ukaguzi wa Ndani na Wahasibu Wakuu wa Wizara na taasisi zake (hawapo pichani) kwenye kikao kazi cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa ripoti ya CAG kilichofanyika Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula baada ya kufungua kikao hicho.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, CPA. Joyce Christopher akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha Wakuu wa Ukaguzi wa Ndani na Wahasibu Wakuu wa Wizara na taasisi zake (hawapo pichani) kuhusu uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa ripoti ya CAG kilichofanyika Dodoma.

Baadhi ya Wakuu wa Ukaguzi wa Ndani na Wahasibu Wakuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na taasisi zake wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa ripoti ya CAG kilichofanyika Dodoma.



Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, CPA. Octavian Barbanas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kikao kazi cha Wakuu wa Ukaguzi wa Ndani na Wahasibu Wakuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na taasisi zake kwa ajili ya uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa ripoti ya CAG kilichofanyika Dodoma.

……………………………………………………………..
Asema Mkaguzi wa Ndani ni Jicho la Taasisi
Awataka Wawe na Uwezo wa Kuzuia Hoja za Ukaguzi Zisitokee
Washauri Mapema na kwa Wakati

Na Prisca Ulomi, WMTH

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula amewafunda Wakuu wa Ukaguzi wa Ndani na Wahasibu Wakuu wa Wizara hiyo na taasisi zake ikiwemo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Baraza la Watumiaji wa Huudma za Mawasiliano Tanzania (TCRA. – CCC), Tume ya TEHAMA (ICTC) na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wakati akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika Dodoma

Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa Wakaguzi Wakuu wa Ndani ni jichola taasisi, ni wasomi, watalaam wa kufanya ukaguzi na kubaini hoja zilizopo ndani ya taasisi hizo na wanawajibika kumshauri mkuu wa taasisi mapema na kwa wakati ili hoja hizo zifanyiwe kazi mapema na kwa wakati na zifungwe ndani ya muda wa mwaka wa fedha husika

Amesisitiza kuwa, “tusisubiri mpaka mgeni aingie ndiyo uanze kusafisha nyumba maana utaacha buibui,” amesema Chaula na kuongeza kuwa ni muhimu kwa Wizara na taasisi zake kupata hati safi badala ya kupata hati chafu au yenye mashaka kutoka Ofisi ya CAG kwa kuwa wao wapo ndani ya taasisi, wanafahamu yanayotekelezwa na taasisi zao na muda wa ukaguzi unajulikana hivyo amewataka wajipange mapema na kuandaa nyaraka za ukaguzi badala ya kusubiri wakaguzi wa Ofisi ya CAG kuibua hoja za ukaguzi

Amewataka wataalam hao kuhakikisha kuwa mipango, mapato na matumizi yanaendana na wakumbuke kuwa Wizara hii ni ya TEHAMA, hivyo wahakikishe wanakwenda na kasi ya ukuaji wa TEHAMA na taratibu za ukaguzi kwa kuwa TEHAMA ni msingi wa maendeleo.

Muandaaji wa kikao kazi hicho, Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo, CPA.Joyce Christopher amesema kuwa malengo ya kikao hicho ni kuhakikisha wataalam hao wanakuwa na uelewa wa pamoja, kubadilishana uzoefu ili kuhakikisha kuwa thamani ya fedha ya miradi ya maendeleo na majukumu yanayotekelezwa na taasisi hizo inapatikana ili Serikali iweze kuhudumia wananchi wake

Akizungumza kwa niaba ya wataalam hao, Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani wa TTCL, CPA. Octavian Barnabas amesema kuwa anaishukuru Wizara kwa kuandaa kikao kazi hicho ili waweze kuwa na uelewa wa pamoja ya kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao.

Wataalam hao watakuwa na ajenda nyingine kwenye kikao kazi hicho ikiwa ni pamoja na kujadiliana kuhusu hoja za CAG za mwaka wa fedha 2019/2020; utekelezaji wa mapendekezo ya CAG kwa mwaka wa fedha 2019/2020; ushiriki wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani katika ufungaji wa hesabu na ukaguzi wa CAG; na uandaaji wa hesabu za mwaka wa fedha 2020/2021.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...