Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said, ambaye ni Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa  maonesho ya 16 ya Vyuo vikuu (TCU),  yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dare es Salaam, ametembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe na  kupongeza  kazi nzuri inayofanywa na Chuo hicho.

 Awali akimkaribisha mgeni rasmi kwenye Banda la Chuo hicho, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, amesema Chuo kimeendelea kuwa mahiri kwa kutoa elimu ya juu na hasa katika maeneo ya Utawala na Uongozi, na kufanikiwa kuzalisha viongozi wengi nchini kwa nafasi mbalimbali, akiwemo Rais wa sasa Mhe. Samia Suluhu Hassan. Amesisitiza Chuo kitaendelea kufanya vizuri zaidi chini ya uongozi wa Mkuu wa Chuo wa sasa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein.

 Akitoa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa kwenye maonesho hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chuo hicho Bi. Rose Joseph, amesema Chuo kinatoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea maonyesho hayo ikiwemo huduma ya ushauri wa kitaalamu kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga kwa program mbalimbali zinazotolewa kwa mwaka wa masomo 2021/22, kufanya udahili (usajili wa moja kwa moja) kwa wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho kuanzia ngazi ya Cheti, Stashahada, Astashada, Shahada za Awali na Shahada za Uzamili (Masters/PhD).

Huduma nyingine ni kupokea ushauri na maoni ya wateja kuhusu kuboresha program na mafunzo yanayotolewa na chuo hicho, pamoja na kuanzisha ushirikiano wa kitaaluma na vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi.

Maonyesho ya 16 ya Vyuo Vikuu nchini yamezinduliwa leo, na yataendelea hadi Jumamosi tarehe 31 Julai 2021, viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said, akikaribishwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka (Mwenye suti kushoto), alipotembelea banda la Chuo kikuu Mzumbe  katika meonesho ya 16  ya Elimu ya Juu , yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam na yatamalizika Jumamosi 31 Julai ,2021 katika viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam.

1.       Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Rose Joseph, akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazoendelea katika  banda la Chuo Kikuu Mzumbe ikiwemo udahili wa moja kwa moja (online application) kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka wa Masomo 2021/22.

Dkt. Thobias Mnyasenga, akitoa maelezo kwa vijana wa kidato cha sita walioonyesha nia ya  kujiunga  na mafunzo ya Elimu ya Juu katika  Chuo Kikuu Mzumbe  walipotembelea Banda la  la Chuo katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Wananchi waliotembelea banda la chuo kikuu Mzumbe wakipata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Mhadhiri  wa Chuo kikuu Mzumbe Dkt.Isaya Lupogo (mwenye shati la kijivu)

1.       Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Rose Joseph, akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazoendelea katika  banda la Chuo Kikuu Mzumbe ikiwemo udahili wa moja kwa moja (online application) kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka wa Masomo 2021/22.

Maafisa kutoka chuo kikuu Mzumbe wakitoa huduma ya udahili wa moja kwa moja kwa waombaji waliotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika  maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...