*Chuo cha CT nchini India kuwafadhili kwa nusu ada

Na Mwandishi Wetu

CHUO Kikuu cha CT kilichoko katika mji wa Punjab nchini India kimetoa ufadhili wa nusu ada kwa wanafunzi 100 watanzania wanaotaka kusomea ufamasia kwenye chuo hicho. Ofa hiyo imetangazwa leo Julai 27,2021 na Mkurugenzi wa  Idara ya Kimataifa ya chuo hicho,  Sourabh  Chaudhary.

Alikuwa akizungumza na wanafunzi na watu mbalimbali wanaotembelea maonyesho ya vyuo  vikuu yanayoendekea kwenye viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam. Chuo hicho na vingine tisa vimekuja nchini kuonyesha kozi wanazotoa kwenye maonyesho hayo kwa mwamvuli wa wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi, Global Education Link (GEL).

Amesema wanafunzi wote 100 watakaopenda kusoma fani hiyo kwenye chuo hicho  watapata punguzo Maalum(Scholarship) hadi 50% na utaratibu wa safari utakuwa mwezi huu wa nane.

Amesema kwa wanafunzi ambao bado wako kwenye mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wao wataingia chuoni kuanzia mwezi wa Tisa.

Sourabh alisema urafiki kati ya Tanzania na India ni wa miaka mingi na kwamba serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa sana katika sekta ya afya hivyo ni dhahiri inahitaji wataalamu wa kutosha kuhudumia sekta hiyo.

Ameongeza kuwa, serikali ya Tanzania imejitahidi pia kuboresha miundombinu kwa wanafunzi wa sayansi wakiwepo hao wanaotaka kusoma kozi za afya.

"Kwa kutumia urafiki baina ya nchi hizi mbili uongozi wa chuo umekubaliana ni vyema kuchagua kozi ambayo ina umuhimu na uhitaji mkubwa katika soko la ajira kwa  kuipunguzia gharama ili Watanzania wengi waweze kuisoma kwa maendeleo ya nchi na taifa kwa ujumla," alisema

Pia amewahakikishia wazazi kwamba kwamba wanafunzi kutoka Tanzania  huwa wanafanya vizuri sana kutokana na maandalizi mazuri yao katika elimu ya sekondari na wengi wao hupokea tuzo mbalimbali kutokana na umahiri wao wa kufanya vizuri,kujishirikisha na michezo na kuonesha tabia njema wawapo chuoni.

Amesema mbali na kozi hiyo ya famasia zipo kozi nyingi akitaja baadhi kuwa ni uhandisi, sanaaa na paramedics  na artificial intelligence kwa uchache.
Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Zena Said akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni kubwa ya uwakala wa elimu nje ya nchi ya Global Education Link (GEL) Abdulmalick Mollel alipotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya vyuo vikuu. Wanaoonekana nyuma ni wawakilishi wa vyuo 10 kutoka nje ya nchi ambao wamekuja kwa mwaliko wa GEL kuonyesha kozi mbalimbali wanazotoa kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea viwanja vya mnazi mmoja.
Wawakilishi wa Chuo Kikuu cha PDEU cha nchini India ambacho ni miongoni mwa vyuo vikuu 10 vya nje ya nchi vinavyoshiriki maonyesho ya vyuo vikuuu yanayoendelea viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kwa mwaliko wa Kampuni ya uwakala wa elimu nje ya nchi, Global education Link (GEL) wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi aliyekuw akitaka maelezo kuhusu chuo chao.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...