Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mkoani Pwani Ridhwan Kikwete akiwa ameambata na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Hajat Mwanaasha Tumbo leo Julai 23,2021 wamefika katika Shule ya Sekondari Kiwangwa na kujionea athari zilizotokana na moto ulioteketeza bweni la wasichana shuleni hapo ambapo wameazimia kurejesha mazingira katika hali yake ya kawaida ili watoto waendelee na masomo.

"Nimefika eneo la Shule ya Sekondari ya Kiwangwa kushuhudia uharibifu uliotokana na Moto uliounguza Bweni la Wasichana shuleni hapo. Shuleni hapo nimekutana na Katibu Tawala wa Mkoa Pwani Hajat Mwanaasha Tumbo. Tumejipanga kudhibiti na kuhakikisha hali inarudi vizuri kimasomo"alisema Mbunge wa Chalinze, Kikwete.

Bweni la wasichana Shule ya Sekondari Kiwangwa, lilishika moto na kuteketea kabisa usiku wa kuamkia leo Julai 23,2021 na hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.
Jengo la Bweni lililivyoteketea
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza na uongozi wa shule na mkoa 

Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza na uongozi wa shule na mkoa 

Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akitembezwa.
Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete akizungumza 
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Hajat Mwanaasha Tumbo (mwenye babibui nyeusi) akizungumza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...