Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WIMBO unaokwenda kwa jina la Twende Tukchanje Mama Hawezi Kumuuza Mwanaye imezindua leo Julai 31,2021 ambapo kwa sehemu kubwa inahamasisha Watanzania kwenda kupata chanjo ambayo sio lazima,ni hiyari.

Akizungumza leo Msanii Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la Mjomba amesema wimbo huo wameshirikiana wasanii watatu ambao ni Barnaba Elias, Felly Kano pamoja na yeye Mpoto na kwamba wameutunga baada ya kujiridhisha na hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan, maelezo ya watalaamu wa afya, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa kutoa ufafanuzi uliowezesha kufanikisha wimbo huo.

"Sisi ni sehemu ya  walando , mimi Mpoto  ni msanii wa kughani muziki na mashairi, niko hapa na wenzangu kama mnavyojua Dunia iko kwenye janga la Corona ambalo ni la kidunia.Ni janga ambalo dunia iliamini linapita lakini bado lipo, watalaam wameingia maabara wametengeneza chanjo.

"Hivyo kwa Tanzania suala la chanjo liko kitaifa, niwakumbushe wakati wa vita dhidi ya Idd Amini wa Uganda kila mwananchi alitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha tunamshinda Nduli Idd Amini, tunakumbuka wanafunzi waliokuwa kidato cha sita wakati ule walihairisha masomo na kwenda kwenye mapambano.

"Tulishinda vita ile sio kwasababu ya mbinu na nguvu zetu bali tulishinda kwasababu ya umoja wa Taifa letu,hivyo kwenye mapambano dhidi ya Corona tunatakiwa kupambana kama Taifa.Tunasisitiza tuko hapa kwasababu Corona ipo na inaua, kuna watu wameguswa, watu wamepoteza familia.Lakini kuna familia hazijaguswa na baadhi yao ndio wamekuwa wakibeza na kuleta mzaha kuhusu chanjo,"amesema Mjomba.

 Hivyo wameamua kutunga wimbo huo kwa kutumia talanta zao kuungana na Rais Samia katika kupambana na Corona."Tumeimba nyimbo mbalimbali lakini sasa tumeona kwa kutumia talanta zetu tunaungane na Rais wetu katika kupambana na Corona,Rais amesema Tanzania sio kisiwa bali ni sehemu ya dunia na kuna muingiliano wa watu."

Ameongeza kwenye  jambo hilo la Corona ni vema Watanzania wakatengeneza umoja wa kitaifa kuishinda Corona huku akifafanua kuna  mambo mengi yanaendelea kuhusu chanjo ya Corona, lakini chanjo haikuanza leo, kuna chanjo nyingi ambazo watanzania wamechanja.

" Hivi kwanini leo hii ndio watumie chanjo kwa ajili ya kuua watu au kuwafanya watu wafe au wawe mazombi, Binafsi nimechanja sina tatizo,nina afya njema, sina shida ya nguvu ya kiume.Hivyo leo tuko hapa kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupata chanjo, wasanii twendeni tukahamasishe.

"Lakini sote tunafahamu chanjo ni hiyari,hakuna anayelazimishwa kwenye chanjo.Rais kama unaniangalia wewe ni shujaa,wewe ni jasiri na tunasema ahsante kwa hatua ambayo umeichukua kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania kwenye janga hili, leo tunazindua wimbo wetu na video itatoka baadae, na baada ya sisi watakuja wasanii wengine nao ambao nao wanaandaa nyimbo zao,"amesema.

Kwa upande wake Msanii Barnaba Clasic, amesema kwamba amefuatilia kwaa kina hotuba ya Rais ambaye amezungumza kwa hisia,ameguwa na ushujaa  wa Rais kuamua  kuchanja hadharani."Hivyo baada ya Rais kuzindua chanjo, nikaongea na Mjomba Mpoto ,nikamuomba tuingie studio ndipo tukarekodi wimbo huu.Wimbo  unaitwa Twendeni tukachanje mama hawezi kumuuza mwanaye.

Amefafanua kuwa mama ndio anayebeba mtoto miezi tisa, ndio anayelea mtoto hadi anakua,hivyo mama hawezi kumuuza mwanaye."Tunawaomba watanzania tukachache, tunajua chanjo ni hiyari, hivyo ni uamuzi wetu na wale ambao wanapotosha kuhusu chanjo.Nawaomba twendeni tukachanje, tumetumia wimbo huu kama fimbo ya kuelimisha na sio fimbo kwa wanaokataa,.

Barnaba amesema kuna ugumu wa kupata chanjo lakini Rais Samia na Serikali yake wamepambana hadi kuipata chanjo, hivyo watanznaia waende wakachanje.

Mrisho Mpoto akieleza jambo wakati wanatambulisha wimbo mpya wa Twende Tukachanje mama hawezi kumuuza mwanaye

Barnaba Elias akisisitiza jambo na hasa akiwahamasisha wananchi kwenda kupata chanjo ya Corona
Barnaba Eliasi ambaye ni mwanamuziki wa muziki wa kizaki kipya( kulia) akifafanua jambo kuhusu wimbo huo.Kushoto ni msanii Mrisho Mpoto' Mjomba'
Msanii Mrisho Mpoto(katikati) akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu  wimbo wao wa Twende tukachanje mama hawezi kumuuza mwanaye.Kulia ni Barnaba Elias na kushoto Felly Kano ambao wameshiriki kutunga na kuimba wimbo huo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalinbali wakimsikiliza Mrisho Mpoto alipokuwa akitambulisha wimbo huo leo Julai 31,2021
Mwanamuzi Felly Kano akizungumza kuhusu wimbo huo wa kuhamasisha watanzani kwenda kuchanja chanjo ya Corona .Wimbo huo wameuzindua leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...