Kushoto ni Mchambuzi wa bajeti -Elimu kutoka Tanzania Youth Vision Association (TYVA), Arif Noorally Fazel akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 24, 2021 wakati wakiwasilisha Uchambuzi wa bajeti kwa jicho la vijana katika bajeti ya 2019/2020  hadi bajeti ya 2021/2022 kwa bajeti ya afya  na elimu. Kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji Tanzania Youth Vision Association (TYVA)- Elimu, Yusuph Bwango.

Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Tanzania Youth Vision Association (TYVA)- Elimu, Yusuph Bwango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 20,2021 wakati wakiwasilisha Uchambuzi wa bajeti kwa jicho la vijana katika bajeti ya 2019/2020  hadi bajeti ya 2021/2022 kwa bajeti ya afya  na elimu. Kulia ni Afisa Miradi kutoka Friedrich Ebert Stuftung (FES), Amon Petro.





KWA mtazamo wa jicho la vijana, juhudi za Serikali kuandikisha watoto kwenye shule za awali na shule za msingi zinaridhisha, isipokuwa malengo ya uandikishwaji hayafikiwi kwa ukamilifu kulingana na malengo. 

Ameyasema hayo na Mchambuzi wa bajeti -Elimu kutoka Tanzania Youth Vision Association (TYVA), Arif Noorally Fazel wakati  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 24, 2021 wakati wakiwasilisha Uchambuzi wa bajeti kwa jicho la vijana katika bajeti ya 2019/2020  hadi bajeti ya 2021/2022 kwa bajeti ya afya  na elimu. 

 Amesema kuwa mtazamo wa jicho la vijana, uchambuzi umebaini kuwepo kwa uwiano hafifu kati ya walimu na wanafunzi.

Uchambuzi uliofanya na TYVA, umebaini kuwa kwa wastani mwalimu mmoja wa shule za msingi anafundisha wastani wa watoto 70, wakati mwalimu wa Sekondari mmoja anafundisha watoto 32.  

"Kutokana na idadi ya wanafunzi na idadi ya walimu, bado kuna pengo katika zoezi la kutoa ajira za waalimu. 

Hivyo Serikali inashauriwa kutenga bajeti zaidi kwa ajili ya kuajiri waalimu  hususani waalimu wa shule ya msingi ambao idadi yao inaonesha kuwa ndogo ukilinganisha na wanafunzi na hivyo kupelekea ukubwa wa majukumu kwa mwalimu mmoja." Amesema Arif Fazel

Pia inashauriwa katika kila mwaka wa bajeti Serikali itoe taarifa Bungeni juu ya Uwiano kati ya walimu na wanafunzi na kutoa taarifa za ajira mpya za walimu.

Kwa upande wa miundombinu TYVA wamebaini kuwa kuna upungufu wa miundombinu ya shule za msingi hususan vyumba vya madarasa, madawati, matundu ya vyoo na nyumba za walimu. 

 Hata hivyo TYVA wameipongeza TAMISEMI kwa kufanya vizuri kutoa mchanganuo wa idadi ya watoto wa kike na wa kiume waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza.

Licha ya TYVA kutoa uchambuzi katika elimu lakini pia wamechambua upande wa afya kupitia Mchambuzi wa bajeti -Afya  Luth Kitentya amesema kuwa serikali na Taasisi ya Chakula na Lishe kutekeleza mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe (2016/2017 – 2020/2021) ambao utekelezaji wake umekoma tangu mwaka wa fedha (2020/2021), Bajeti haijaakisi namna ya kutekeleza mkakati wa kuelimisha jamii juu ya lishe bora na athari za utapiamlo kwa jamii.

Hata hiyo amesema kuwa Serikali inashauriwa kutenga fedha mahususi ili kufanikisha kampeni za kuhamasisha jamii juu ya lishe bora na umuhimu wake na kutoa elimu juu ya namna ya kuandaa chakula lishe chenye tija kwa afya za jamii.

"Licha ya Serikali na wadau wa maendeleo kutoa elimu na umuhimu wa kupima afya, kumekuwa na upungufu mkubwa wa wanaume kutoshiriki kwenye kupima VVU. Ukilinganisha na ongezeko la 2015/2016 hadi desemba 2019 serikali ilibainisha kwenye bajeti ya 2021/2022 namna itakavyopambana kudhibiti UKIMWI na maambukizi mapya." Amesema Kitentya

Pia amesema Serikali inashauriwa iongeze juhudi kwenye mapambano ya udhibiti wa janga la VVU/UKIMWI na kutoa elimu kwa vijana, umma wa Watanzania na jamii nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...