Mbunge wa Jimbo la  Bumbuli January Makamba ameahidi Kuendelea kulipigania na kulipeleka Bungeni  suala zima la Changamoto ya barabara lilopo maeneo ya vijijini  ili  kuwepo usawa kati ya mjini na vijijini.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mponde  kuhusu Serikali ya  awamu ya sita ilivowapatia sh. 1.5 9 bilion kwa ajili ya kujenga  Barabara kwa kiwango cha lami  na changarawe  kwenye baadhi  ya Barabara  zilizopo kwenye Jimbo hilo.

Makamba alitaja barabara zitakazonufaika na fedha hizo  kwa kujengwa kwa kiwango cha changarawe kuwa ni Barabara   ya Mgwashi - Mbelei yenye urefu wa kilometa 23.8 ,Bumbuli -Mayo, Vulii- Mahezangulu  hadi Magoma kilometa 15.4,Vuga - Mponde hadi Wena kilometa 21.2 na Balangai - Tamota na Vuliii  yenye urefu wa kilometa 13.4,Soni -Mponde kilometa 13.4 pamoja na Bumbuli center itakayojengwa kwa kiwango cha lami.

Mbunge huyo alisema sio sawa kuona  mjini wanajengewa barabara za juu na zinapanuliwa kila kukicha lakini vijijini ambako wapiga kura wengi wapo, wanapata shida kupitisha mazao yao kutokana  na barabara  kuwa changamoto  hasa wakati wa  msimu wa mvua.

" Inauma mtu analima chai yake anapalilia mwenyewe  lakini anashindwa kupeleka kiwandani sababu barabara inautelezi hii sio sawa kabisa" alisema  Makamba

"Mimi huwa nawaambia wenzangu kama kweli tunaweka  barabara za maghorofa hatushindwi kuwasaidia watu wa vijijini kwani wanachotaka barabara zao zipitike wakati wote hasa kipindi cha mvua" Alisema Makamba

Alisisitiza kuwa  lazima kuwepo na haki sawa katika kupeleka maendeleo ya nchi  ,haiwezekani kwa Dar es Salamu tu kuna barabara moja ina njia nne mpaka sita  ambapo  alitolea mfano yaani  barabara moja ni kama  kiwanja cha mpira yaani barabara  inakuwa kwenye kona ile na kona nyingine.

Aidha  alieleza kuwa moja ya malengo makubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kupambana na barabara za vijijini.

Aliongeza kwamba serikali imepanga ifikapo mwaka  2025 Watanzania wanaokipigia chama cha Mapinduzi kila mwaka angalau barabara zao ziwe zinapitika wakati wote sababu hao tunaowajengea za magorofa yawezekana  baadhi yao hawapigi  ata kura wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo alisema  yeye kama Mbunge kiu yake ni kuona wananchi wake wanaondokana na changamoto hiyo ambayo ni kero kubwa ukilinganisha na jiografia ya maeneo ya Jimbo la Bumbuli

Makamba ameanza rasmi ziara ya kukagua miradi ya maendeleo  na kuweka mawe ya msingi katika Jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akikagua Maabara ya sayansi katika shule ya sekondari ya kiviricha kata ya Usambara iliopo Halmshauri ya Bumbuli Mkoani Tanga ambayo zahanati hiyo Mbunge ameichangia mil.10,Wananchi milion 25 na serikali kuu Milion 35 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...