*RC: Wekezeni katika miradi rafiki

*Msikurupuke kuanzisha miradi, jifunzeni kwanza

*Aipongeza PSSSF kwa semina

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewashauri Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwekeza katika miradi waliyoizoea ili waweze kuindesha vyema na kwa faida.

Mhandisi Gabriel alisema hayo Jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wastaafu watarajiwa kwa wanachama wa PSSSF wa mkoa wa mwanza inayofanyika Julai 26 hadi 27, 2021.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, akihutubia wakati akifungua semina ya Wastaafu watarajiwa wa PSSSF. Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi na katika ni Bi. Nyamisinda Manyunyi kutoka NMB.

“Kama unataka kuingia katika mradi wowote, hakikisha unaonana na wataalamu ili waweze kukusaida katika uwekeza sahihi na wenye tija,” alisauri Bw. Gabriel

Aliwashauri wastaafu hao watarajiwa watakapolipwa mafao yao wasikurupuke kuanzisha miradi bali yajifunze vyema mradi wanaotaka kuwekeza ili wajue njia sahihi ya kuwekeza katika mradi huo

“PSSSF wameletea Mabenki na Taasisi mbalimbali ili muweze kupata uelewa na maarif ili mfanye maamuzi sahihi ya uwekezaji. Hivyo tumieni fursa vyema, hii bahati kubwa kwenu, kwani sio wote wanaopata fursa kama hii,” alisema Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel (Wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Taasisi za fedha zinazoshiriki semina ya Wastaafu watarajiwa wa PSSSF mkoa wa   Mwanza.

Alisema ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza itatoa elimu na ushauri bure katika kuhakikisha Wastaafu wa mkoa wa Mwanza wanafanya uwekeza sahihi kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza awali wakati akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa mwanza, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha Bi. Beatrice Musa-Lupi alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali mwaliko wa kufungua semina hiyo kwa wastaafu wa mkoa wa Mwanza.

Wastaafu watarajiwa wa Mkoa wa Mwanza, wakimsalimia Mkuu wa mkoa wa Mwanza (hayupo pichani)

Azishukuru taasisi za fedha zikizofanikisha kufanyika kwa semina hiyo, taasisi hizo ni CRDB, NMB, TCB, NBC, DCB, BENKI ABC, BENKI YA AZANIA, MCB na UTT AMIS. Alizishukuru pia kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wastaafu watarajiwa wa PSSSF. Taasisi nyingine zinazotarajiwa kutoa elimu ni SIDO, TAKUKURU na TCRA.

Akizungumzia semina hizo kwa wastaafu, Bibi Musa-Lupi alisema, “Semina hizi ni endelevu, na zitaendeshwa kila mwaka kwa wanachama wa PSSSF waliobakiza kipindi kisichozidi miaka miwili kabla ya kustaafu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...