Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Andrea Pembe amesema chuo chake kimekuwa kinafanya kongamano la kisayansi kuhusu tafiti mbalimbali kwa mwaka wa tisa mfululizo.

Prof Pembe amesema kuwa, tafiti hizi zimekuwa zinatumika katika utungaji wa sera za kiafya ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa wakati wa kufungwa na Kongamano la kisayansi lililofanyika kwa siku mbili katika Chuo cha MUHAS lililowakutanishwa wataalam mbalimbali na watafiti, watunga  sera na watekelezaji wa huduma za afya.

Prof Pembe amesema, kongamano hilo limekuwa linaangalia masuala mbalimbali hususani magonjwa yasiyoambukiza yaliyopo na yanayoendelea kujitokeza kila siku.

Amesema, katika kongamano hilo watafiti wameangalia changamoto zinazoikumba jamii na namna wanaweza kuwa na fursa kwenye kutafuta ufumbuzi utakaokuwa na tija kwa taifa na hata nje ya nchi.

“Tumeangalia tafiti mbalimbali juu ya ugonjwa wa Uviko 19 na magonjwa mengine yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu na kansa na namna gani ya kupambana nayo kisayansi.” Amesema Prof Pembe.

“ Kuna habari mbalimbali zimekuwa zinasemwa hazina ukweli wowote na MUHAS tumekuwa tunatoa taarifa mbalimvali kwa jamii ambazo ni sahihi kuhusu Uviko 19,” amesema


Prof Pembe amesema, katika kipindi cha miaka ya 2007 hadi 2012 kuliwahi kutokea milipuko ya homa ya mafua ya mapafu na mediteranea na watafiti walipambana kupata suluhisho la ugonjwa huo.

Amesema, katika chanjo nane ambazo zinatumika kwa sasa za Uviko 19 zote ni salama na zimethibitishwa na Shirika la afya duniani (WHO) na chanjo hizi zimekuwa zinasaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa wa Uviko 19 na inamsaidia mgonjwa kutokulazwa au kuwekewa mashine ya kupumua.

Kongamano hilo la kisayansi limeweza kuhudhuriwa na watafiti mbalimbali wa ndani na wa kimataifa na yamekuwa na mchango mkubwa kwa sekta ya afya nchini.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Andrea Pembe akizingumza wakati wa ufungaji wa kongamano la Kisayansi linalofanyika kwa mwaka wa tisa likifanya tafiti na utangaju wa sera za kiafya kwa magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Andera Pembe akimtunuku tuzo moja ya watoa mada wakati wa Kongamano la Kisayansi lilizungumzia masuala mbalimbali ya kitafiti kuhusu magonjwa yasiyoambukiza pamoja na Ugonjwa wa Uviko 19 na namna ya kupambana na changamoto zake.

Washiriki mbalimbali wa Kongamano la tisa la Kisayansi lililofanyika kwa muda wa siku mbili likihudhuriwa na watafiti mbalimbali, watunga sera na watoaji wa huduma za afya


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...