Na Gift Thadey, Babati

TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Manyara, kwa kipindi cha miezi mitatu ya Aprili hadi Juni mwaka huu, imekagua utekelezaji wa miezi 15 ya maendeleo ya thamani ya shilingi bilioni 2.27.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo Mjini Babati ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu.

Makungu amesema lengo la kukagua miradi hiyo kwenye mkoa huo wa Manyara ni kujiridhisha na ubora ikilinganisha na thamani ya fedha iliyotumika.

Ametaja miradi iliyofanyiwa ufuatiliaji ni ujenzi wa uzio wa Ikulu ndogo ya Hanang’ wenye thamani ya shilingi 250,000,000 na ujenzi wa miundombinu ya shule mpya ya sekondari Lalaji wa thamani ya shilingi 700,000,000.

Ametaja miradi mingine ni ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya Mogitu ya thamani ya shilingi 400,000,000 uliokataliwa kufunguliwa na Mwenge na kuagiza TAKUKURU Mkoa wa Manyara ichunguze.

“Uchunguzi wa TAKUKURU umeonyesha hakuna ufujaji wa fedha uliofanyika na tumejiridhisha kuwa umejengwa kwa ubora na una akisi thamani ya fedha iliyotumika,” amesema Makungu.

Amesema changamoto iliyojitokeza ilitokana na mapungufu katika uandaaji wa taarifa iliyosomwa kwa kiongozi wa mbio za mwenge Luteni Josephine Mwampashi.

Amesema uchunguzi umebaini muadnaaji wa taarifa hiyo hakuwa na taaluma stahiki ya usimamizi wa fedha hivyo alichanganya fedha za mradi huo na fedha za miradi miwili ya kijiji.

Ametaja mradi mwingine ni ujenzi wa choo na miundombinu ya zahanati ya Dawar wa shilingi 22,000,000 na ofisi ya udhibiti ubora shule wa halmashauri ya mji wa Mbulu shilingi 42,270,315.

“Mradi mwingine ni ujenzi wa bweni na nyumba ya walimu Maretadu wa thamani ya shilingi 175,000,000 na ofisi ya udhibiti ubora shule wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu shilingi 181,818,181,” amesema Makungu.

Amesema mradi mwingine ni ujenzi wa zahanati ya Njia panda ya shilingi 139,000,000 matundu 10 na madarasa manne shule ya Kaloleni shilingi 47,700,000 na choo cha zahanati ya kijiji cha Njoro wa shilingi 19,000,000 maabara Kibaya shilingi 30,000,000 na madarasa saba na choo shule ya msingi Endahagichan shilingi 47,700,000.

Ametaja mradi mwingine ni na ujenzi wa madarasa mawili na matundu nane ya vyoo shule ya msingi Kiru Six wenye thamani ya shilingi 48,880,000 ujenzi wa wodi ya wazazi ya hospitali ya Mrara shilingi 400,000,000 na mradi wa mitaro ya barabara ya Kibaya ya thamani ya shilingi 278,268,970.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...