Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya amesema tusipochukua  hatua thabiti za kupambana na ugonjwa wa corona , yanaweza kutokea maafa makubwa zaidi.

 Waziri Mkuu huyo Mstaafu ameyazungumza hayo leo Julai 24, 2021,  akiwa Mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga wakati akitoa hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM  Wilayani hapo

"Ni muhimu  tukumbushane  kuhusu maelekezo ya Serikali yetu ya  awamu ya sita juu ya mchakato wa kupambana na gonjwa hili la corona, uginjwa huu umetikisa Dunia nzima na umeendelea kusambaa," - Msuya.

" Nchi yetu Tanzania tumeathirika kwa kiasi, lakini kama hatua thabiti hazitachukuliwa janga linaweza kuwa kubwa zaidi,  tufuate maelekezo yanayotolewa na viongozi wetu pamoja na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka au kutumia sanitizer pamoja na kuepuka misongamano, isiyokuwa ya lazima" - Msuya

Msuya  amesema kanuni hizo za kujikinga na kujilinda na corona,  ziendelee kuzingatiwa katika nyumba za ibada, mashuleni, vyuoni, nyumbani na kwenye vyombo vya usafiri kujikinga ni muhimu kuliko tiba" - Msuya

Waziri Mkuu huyo Mstaafu ameutaka mkutano mkuu huo, kutoa tamko la kuomba viongozi wa nyanja zote kushawishi wananchi kuchukua tahadhari na kutekeleza hatua zote za kujikinga na ugonjwa huo hatari na kusisitiza mtu ambaye hatazingatia hatua za kinga atapata maafa.

"Nchi nyingi duniani zimetikiswa na gonjwa hili, sisi sio kisiwa, hivyo Tanzania kama moja ya jamii duniani, inashiriki kwenye maelekezo haya kwa wananchi wake, viongozi wametoa na wameendelea kushauri la kufanya ili kuepukana na janga hili la corona, wananchi itikeni wito huu kwa vitendo."

Naye Mwenyekiti wa CCMia Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi amesema suala la kuchukua tahadhari ya "corona lisiwe jambo la kubembelezana ni lazima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...