Mchambuzi wa bajeti -Afya kutoka Tanzania Youth Vision Association (TYVA), Luth Kitentya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wakiwasilisha Uchambuzi wa bajeti kwa jicho la vijana katika bajeti ya 2019/2020  hadi bajeti ya 2021/2022 kwa bajeti ya afya  na elimu.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Tanzania Youth Vision Association (TYVA)- Elimu, Yusuph Bwango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 20,2021 wakati wakiwasilisha Uchambuzi wa bajeti kwa jicho la vijana katika bajeti ya 2019/2020  hadi bajeti ya 2021/2022 kwa bajeti ya afya  na elimu. Kulia ni Afisa Miradi kutoka Friedrich Ebert Stuftung (FES), Amon Petro.


UCHAMBUZI wa jicho la vijana katika  bajeti ya 2019/2020  hadi bajeti ya 2021/2022 afya
umebaini kuwa kumekuwa na upungufu wa vifo vinavyotokana na malaria, ambavyo vingeweza kuathiri vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa. 

Ameyasema hayo Mchambuzi wa bajeti -Afya kutoka Tanzania Youth Vision Association (TYVA), Luth Kitentya leo Julai 24, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wakiwasilisha Uchambuzi wa bajeti kwa jicho la vijana katika bajeti ya 2019/2020  hadi bajeti ya 2021/2022 kwa bajeti ya afya na elimu.

Pia amesema kuwa katika juhudi za Serikali kupambana na Malaria kumeonekana mafanikio katika kupunguza visa vipya (Incidences) kwa asilimia 35 na idadi ya vifo kwa asilimia 61.

"Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imeendelea kuhakikisha kuwa, dawa za kutibu malaria na vitendanishi zinapatikana wakati wote kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya." Amesema Kitentya

Amesema kuwa Kwa kipindi cha Mwezi Julai 2019 hadi Machi 2020, Wizara imenunua na kusambaza Dawa Mseto (ALu) dozi 8,228,910, Sindano Artesunate vichupa 1,624,985 sawa na asilimia 100 ya mahitaji kwa ajili ya Malaria kali (severe Malaria) na Vitendanishi 32,220,900 ambazo zimewafikia wananchi kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya.

" Asilimia ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na vimelea vya malaria kwa kutumia vipimo vya mRDT imeongezeka hadi kufikia asilimia 98 mwezi Machi 2020 ikilinganishwa na asilimia 95 mwaka 2015/16. Ongezeko hili limetokana na uhamasishaji wa jamii ili kutambua umuhimu wa kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kuthibitisha uwepo wa vimelea vya Malaria kabla ya kutumia dawa kwa kutumia kaulimbiu ya “Sio kila homa ni Malaria”. Maambukizi ya Malaria yamepungua kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 7.3 Machi 2020." Amebainisha Kitentya

Aidha Kitentya amesema kuwa vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kutoka vifo 6,311 mwaka 2015 hadi kufikia vifo 2,079 Machi 2020.

Hata hivyo ameishauri Serikali kuendelea na mapambano ya udhibiti wa Malaria nchini, ili kufikia Tanzania bila malaria. Pia kutoa elimu kwa jamii juu ya namna bora ya kukabiliana na malaria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...