Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Paris kilichopo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo ambapo amewataka kutowaficha wahalifu wanaohatarisha usalama wao.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Abubakari Akida,MOHA
WANANCHI wa kijiji cha Paris kilichopo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar wametakiwa kutowaficha wahalifu wanaopatikana katika maeneo yao ili kuweza kuishi kwa amani na salama ili lengo la nchi kuendelea kiuchumi litimie.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho kwenye Mkutano wa Hadhara ambapo kabla ajazungumza nao alipata nafasi ya kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi hao.

Amewataka wananchi hao kutoyafumbia macho matendo ya uhalifu ikiwemo uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya,matendo ya udhalilishaji,uporaji na wizi

“Kuna wengine wamesema yapo matukio ya kihalifu hapa yanafanyika, watu wanaiba hapa, watu wanatembea uchi, bangi zinauzwa hapa, sasa akitokea mtu anatokea sehemu ya mbali kama mlivyosema anafanya matendo ya uhalifu basi mripoti kwa Jeshi la Polisi,mkishajua huyu ndio muuza unga maarufu hata mimi niambieni nitawatauma askari wangu waje wamshughulikie,msimpige wala msichukue sheria mkononi chukueni hatua za kinidhamu na kisheria sio mumpige mtakuja kutengeneza balaa linguine” alisema Naibu Waziri Chilo

Awali mkazi wa Kijiji hicho Said Mpangaleni akizungumza katika mkutano huo amesema kuwepo kwa uhalifu uliokithiri katika Kijiji chao imepelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo watu wakihofia usalama wao

“Hapa pana genge la uuzaji na utumiaji dawa za kulevya na ndio linaratibu uhalifu wote katika Kijiji hiki,mtu akishakula maunga yake kinachofatia ni uhalifu tu kwa kweli tumekua tukiishi kwa hofu,bora sisi wanaume tuna afadhali lakini dada zetu wanaporwa mchana kweupe,serikali itusaidie kwenye hili kwani kwa hali hii huo uchumi tunaoambiwa hatuwezi kuupata hali huku ni tete” alisema Said

Wakitoa neno la shukrani baada ya mkutano huo wawakilishi wa wananchi hao wameiomba serikali kufungua kituo cha polisi katika maeneo hayo kwani itarahisisha udhibiti wa uhalifu katika Kijiji chao hali itakayopelekea kustawi kwa amani huku pia wakiomba kuongezwa kwa askari wa ulinzi shirikishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...