Na John Walter-Babati


Jukwaa la wanasayansi vijana kutoka shule mbalimbali za Sekondari katika mkoa wa Manyara wameiomba serikali kuanzisha mtaala mpya ambao utasaida kupunguza au kuondoa kabisa janga la ukosefu wa ajira nchini.
 
Wameyazungumza hayo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza na  kuwakabidhi vyeti pamoja na  medali baada ya kushinda katika mashindano ya Vijana wanasayansi mkoani hapo (YOUNG SCIENTISTS ) iliyofanyika shule ya sekondari Bagara mjini Babati.
 
 Wanafunzi hao wamesema wakiungwa mkono kuanzia ngazi ya sekondari katika kufanya tafiti mbalimbali kutawafanya kuwa wabunifu wa kisayansi na kiteknolojia hali itakayochagiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
 
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Bagara, Ushindi Isaya anasema wao waliona ongezeko la watu waliokosa ajira ni kubwa hali inayopelekea kufanyika kwa vitendo viovu kwenye jamii hivyo kuwepo kwa mtaala ambao utaelekeza wanafunzi kupewa ujuzi wa jambo Fulani utakuwa muarobaini wa changamoto hiyo.
 
Alisema anaiomba serikali ilete mtaala mpya ambao utamwezesha kila mhitimu  kujiajiri mwenyewe Mkuu wa wilaya ya Babati Lazari Twange amesema jukwaa hilo likisimamiwa vyema litaongeza idadi ya wananfunzi wanaosoma masomo ya Sayansi ambao ndani yake watapatikana  wahandisi na wabunifu vijana ambao wataongeza msukumo katika sayansi na teknolojia nchini.
 
Amesema Fursa za kazi zitakuwepo kwa wahitimu kwa kuwa watakapohitimu watakuwa na uwezo wa kujiajiri kutokana na uwezo walioupata.
 
Mwalimu Jackson Warae aliefanya kazi na Vijana wanasayansi kwa miaka sita anasema ameshiriki katika kuibua vipaji vya wanafunzi ili kuongeza utafiti katika nchi ya Tanzania ambapo  wanafunzi wawili wa shule ya Sekondari Chief Dodo walishiriki mashindano na kuwa washindi wa kwanza kitaifa kwa mwaka 2019  ambao pia walipata nafasi ya  kuiwakilisha nchi katika mashindano ya afrika yaliyofanyika Afrika ya Kusini  na kushika  nafasi ya kwanza kwenye kipengele cha Kilimo (AGRICULTURE) kwa kuwasilisha teknolojia yao ya kuwaingiza nyuki kwenye mzinga bila kusubiri majira ya maua.
 
Mwalimu Kwaraye anasishauri serikali iwezeshe wanafunzi wa ngazi ya sekondari kuwa wadadisi na watafiti ili  kuisaidia jamii katika mambo mbalimbali na kuyapatia ufumbuzi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...