Na Mwandishi wetu

ASASI za kiraia nchini zimetakiwa kushikamana kwa pamoja na kuhakikisha wanazisemea kazi wanazofanya katika taasisi zao ili zifahamike kwa wananchi na jamii kwa ujumla.

Pia asasi hizo zihakikisha zinaangalia mifumo mbalimbali inayowaongoza ambayo ndio miundombinu ya uwajibikaji katika kazi zao hususani katika kutatua matatizo ya wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati mpya wa Foundation For Civil Society (FCS) RAIS wa Taasisi hiyo Dkt. Stigmata Tenga amesema kuwa Asasi za Kiraia zinapaswa kujengwa kutokana kuwa ni muhimili mkubwa wa maendeleo nchini nakwamba wananchi wanapaswa kuzifahamu.

“Tuisemee sekta hii na yale yote ambayo sekta hii inayafanya kwenye jamii, yasemeeni mnayoyafanya ili yajulikane msione aibu yeyote,”amesema Dkt. Tenga na kuongeza Asasi zinapaswa kutatua matatizo ya wananchi na kusaidia kuyaondoa, hilo ndio lengo kubwa la FCS katika Dira yake.

“Tujenge uwajibikaji katika misingi ya ubinadamu na utu bila kujali kuna nini, bali kuwashirikisha  wenzetu matatizo ambayo sekta ya Asasi za kiraia nchini inapitia  ambayo yanahitaji kutatuliwa kwani ni matatizo yanayojikita katika mifumo,”amesisitiza Dkt. Tenga

Aidha amesema hawapaswi kutatua  matatizo kwa mbinu zile zile za zamani ambazo sio mbinu za kujenga mifumo bali ni mbinu za kutoa huduma.

“Tusipoangalia hivyo tutazidi kuona hizo mbinu zinaongezeka na kuwa kubwa sana  na kuhakikisha wanaangalia mifumo ambayo ndio miundombiniu ya uwajibikaji katika Aaasisi,” alisema

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji  wa FCS Francis Kiwanga amesema kuwa wamezindua mpango mkakati mpya wa FCS
ambao unalenga kushuka chini hususani vijijini katika kuwasaidia wananchi.

Ameongeza kupitia mpango huo Taasisi yao itaendelea kufanya kazi na Asasi mbalimbali za kiraia ambao ndio wadau wao muhimu katika kuwafikia wananchi.

Pia falsafa ya taasisi yao inaamini kuwa umasikini,hali ya kutokuwa na haki katika jamii,hali ya ukandamizaji watu wengine ni tatizo kubwa na ni adui wakubwa wa maendeleo.

Amesema katika rasilimali zao takribani asilimia 90 inakwenda vijijini kuhudumia wananchi “Rasilimari zetu tunavyogawa kila mwaka asilimia 90 inakwenda vijijini tunaamini waliopo Dar es Salaam ,Taasisi  nyingi zinaweza kufanya kazi na watu wengine kokote duniani,kuliko waliopo vijijini” alisema Kiwanga

Ameongeza katika mpangokazi wao wanazingatia usawa wa kijinsia,kufanya kazi na wadau wao kuwapa heshima inayostahili  na kuwaheshimu kwani wao ndio wabia wao wakubwa na kwamba sauti yao ina ukubwa wa kuweza kuwafikia wananchi wengi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi za kiraia, Dkt.Richard Samabiga ameipongeza FCS kwa hatua hiyo ya kuzindua mpango mkakati huo ambao unaonyesha dira ya kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali.Mpango huo unaleta matumaini makubwa kwa Asasi za kiraia katika kufanya kazi zao za kusaidia wananchi.

"Huu Mpango mkakati umejikatika katika kutekeleza miradi ya utawala bora,  usawa wa kijinsia na watu wenye ulemavu, kukuza uchumi na kujenga amani na utatuzi wa migogoro,"amesema.

Mkurugenzi wa FCS Francis Kiwanga (wa tatu kulia) akiwa na Rais wa Taasisi hiyo Stigimana Tenga (katikati) na mwenyekiti WA WA Bodi ya FCS DKT.Richard Samabiga (wa kwanza kulia) wakiangalia mpango mkakati utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano mara baada ya kufanyika uzinduzi rasmi wa mpango huo uliofanyika kwenye ofisi za FCS Jijini Dar es Salaam,
Rais. wa FCS Dkt. Stigimana Tenga akizungumia mpango huo mara baada ya kuzinduliwa rasmi
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo akielezea namna ambavyo FCS itavyotekeleza majukumu yake Katika kuusimamia mpango huo
Baadhi ya watumishi wa FCS na wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango huo
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...