Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB) akihutubia wageni waalikwa wakati wa kumpongeza na kumuaga Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, ambae amemaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho hafla hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana.


Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, akizungumza wakati alipokuwa akiwaaga wafanyakazi wa chama hicho pamoja na wadau mbalimbali baada yakumaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho, katika hafla hiyo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama hafla hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Chama cha Waajiri Tanzania ATE  Wakili Suzanne Ndomba,  akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumpongeza na kumuaga Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama hicho Dkt. Aggrey Mlimuka, ambae amemaliza muda wake wa utumishi wake  hafla hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB) (wapilikushoto), akikabidhi zawadi kwa Mkurungezi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, iliyotolewa na Chama hicho wakati wa hafla ya kumpongeza na kumuaga mara baada yakumaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chama hicho Bi jayne Nyimbo pamoja na Mke wa Dkt. Aggrey Mlimuka.
 


CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanikisha tukio kubwa na la kihistoria katika utaratibu wake wa kupokezana uongozi wa ngazi za juu, ambapo Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji Dk. Aggrey Mlimuka anastaafu na kutoa  fursa kwa awamu mpya ya uongozi chini ya mrithi wake, Suzanne Ndomba.

Pamoja na mabadiliko hayo ni jambo la  kujivunia kwamba katika uwepo wake, ATE imefanikiwa katika kupevuka kishughuli kiasi cha malengo yake kupanuka zaidi ya lile la kudumisha uhusiano kazini, na sasa ni mdau thabiti katika kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara Tanzania yanaboreshwa.

Pamoja na hayo, ATE kama taasisi mama inayounganisha waajiri imefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama, na vilevile imekuwa ikiibua miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa kushirikian na wadau nawashirika mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake Dk. Aggrey Mlimuka alisema : “ Mafanikio yaliyofikiwa katika awamu yangu ya uongozi yamewezekana kutokana na ushirkiano wa uongozi    wa sasa na uliopita, pamoja na bodi, na nina wiwa kuona nao pia wanapokea shukurani zao zinazostahili”

Dk.Mlimuka alibainisha kuwa ATE inazo changamoto zake zandani ya taasisi, mojawapo na kubwa zaidi ni ulipaji mdogo wa ada za wanachama. “ Tunatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye vyanzo vyetu vya fedha na kuondoa hali ya sasa ambapo pamoja na kwamba ATE ni chama chenye wanachama matajir ilakini  chenyewe kinabakia kuw nimasikini” alisema Dk Mlimuka.

Kama taasisi inayojihusisha na ajira, ATE inaona haya ya sheria za nchi kuhusiana na maswala ya ajira kufanyiwa mabadiliko ili kuendana na hali halisi ilivyo duniani, hasa kutokana na mabadiliko yaliyoletwa na utandawazi. “ Sheria zetu zimepitwa na wakati na hazishabihiani na haliiliyopo. Baadhi ya sheria zilitungwazaidi ya miaka 17 iliyopita na zina mapungufu. Sheria za ajira  hazina budi kuendana na hali halisi ya kisiasa na kiuchumi”, alisema Dk. Mlimika.

“ Nina matumaini kuwa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini itafanyiwa marekebisho yapasayo ili kuboresha na kuleta ulinganifu katika wajibu na haki za waajiri na wafanyakazi. Natumaini vilevile kuwa ATE  itashiriki ipasavyo na kutoa mchango ili kurekebisha hali hiyo na hivyo kusaidia kupanua ajira. Waajiri hawana budi sasa kuitambua ATE.”

Taasisi ya ATE  bado itaendelea kuimarisha uhusiano kati yake na serikali na wafanyakazi. Maboresho hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza ufanisi kazini, kuongeza kipato cha wafanyakazi na kwa upande wao wafanyakazi watazalisha zaidi, kodi itaongezeka  na kufanya hali ya kifedha ya serikali iimarike. Kuboresha uhusiano kutasaidia kuwepo kwa ajira endelevu na ya uhakika. Wafanyakazi wote katika sekta zote bila kubagua watafaidika na mahusiano mazuri maeneo ya uzalishaji.

Alisema Dk Mlimuka : “ Hadi sasa uhusiano na serikali umekuwa ni mzurisana, kwa kuwa ATE imekuwa ikifanya kazi kwa karibu zaidi na wizara mama, viongozi wa ngazi za juu wa serikali  na muungano wa wafanyakati yaani TUCTA.  Kwa mfano, ATE ni mjumbe wa bodi mbalimbal I za taasisi za umma.”

Kwa upande wa miradi, ATE imekuwa ikiendesha program za  kuzuia ajira za watoto kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya watoto, yaani UNICEF. Vilevile ATE imekuwa ikishiriana na vyama visivyokuwa  vya kiserikali ili kuongeza tija kwa walemavu na kuwaandaa wawe na sifa za kuajirika. Eneo lingiine limekuwa ni katika kuwawezesha wanawake kushika nyadhifa za uongozi,  ambapo mafunzo mbalimbali yamekuwa yakiendeshwa kwa lengo la kuwapa wanawake sifa  zitakazowawezesha kukwea hadi ngazi za juu kabisa za uongozi.

Alisema Mlimuka, “ Kwa siku za usoni, tunategemea kupanua wigo wa mradi huu wa wanawake kujumuisha wanasiasa, ambapo tumepanga kuendesha mafunzo kwa Wabunge wanawake kwa upande wa Tanzania Bara na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Visiwani.”

Hivyo basi, ikiwa imejipanga vyema kutekeleza malengo yake, ATE leo inastahili kuwa na fahari wakati inamkaribisha Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji mpya, Suzanne Ndomba, ambaye ni matokeo ya program hiyo ya ATE ya kuwawezesha  wanawake na kuwaweka tayari kushika nyadhifa za juu za uongozi.

“ ATE imefanya kwa vitendo falsafa yake kwa kutumia mafunzo hayo vyema. Nikiwa moja wa waliofaidika na program hiyo, itoshe kusema tuna uwezo, weledi, uzoefu na sifa ambavyo vinatuwezesha kushika nyadhifa za juu za unongozi vyema,” alisema Suzanne Ndomba. “ Nina msimamo wangu na nina uwezo wa kufanya maamuzi, hata hivyo ninakaribisha maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali. Uongozi unahitaji ushirikiano, na kiongozi si lazima  awe anafahamu kila kitu.”

Akigusia kuhusu dira ya ATE, Suzanne alisema dira hiyo imebeba azma ya ATE ya kuhakikisha inatoa mchango kwenye kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. “ Tutahakikisha tunatekelzea dira hiyo, na nichukue fursa hii kuwahakikishia wadau ya kuwa ATE itaendelea kuwa sauti ya waajiri Tanzania,” alisema.

“Tutaendeela kufanya kazi kwa karibu zaidi na serikali katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Kwa Upande wetu, ATE tunaridhishwa na hatua ambazo zimekwisha chukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania.”

Kuhusiana na kupanua wigo wa wanachama, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji mpya Suzanne Ndomba amesisitiza haja ya waajiri kujiunga na ATE.  Alisema kama taasisi mama inayounganisha waajiri wote, shughuli za ATE  zinazaa manufaa yasiyobabu ambayo mwisho  siku yananufaisha waajiri wote katika sekta zote.

“ Hivyo basi, natoa wito kwa waajiri wasio wanachama kujiunga na ATE na kuongeza nguvu kwenye utakelezaji wa malengo yake. Ili ATE ifanikiwe, inatakiwa waajiri wote wawe wanachama wa taasisi hii,” alisema Suzanne. “ Mimi kama Mkurugenzi  Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji  mpya  nitahakikisha kuwa  naongeza idadi ya wanachama kwa kuhakikisha kila mwajiri anakuwa mwanachama wa ATE.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...