Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua Majengo katika Chuo cha Ualimu SHYCOM.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amekagua ujenzi na ukarabati wa majengo, katika Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM), na kuagiza Mkandarasi akamilishe mapungufu yaliyopo, zikiwemo nyufa ndogo ndogo.

Mboneko amefanya ziara hiyo leo akiwa ameambatana na viongozi wa Serikali, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.
Mboneko alisema Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sanyansi na Teknolojia, ilitoa kiasi cha fedha Sh. bilioni 9.8 kwa ajili ya kukarabati na kujenga majengo katika chuo hicho cha Ualimu Shycom, ili kuboresha mazingira mazuri ya kusomea wanafunzi.

"Leo nimefanya ziara ya kukagua ukarabati na ujenzi wa majengo katika chuo hiki cha Ualimu Shycom, ili kuona maendeleo yake, na kuhakikisha kama wanafunzi wameanza kuyatumia," alisema Mboneko.

"Serikali tumekarabati na kujenga mabweni, madarasa, vyoo, nyumba za walimu, bwalo, Maktaba ya vitabu, jengo la midahalo,pamoja kujenga tenki la maji lita 300,000 , na kumaliza changamoto ya maji chuoni hapo," aliongeza.

Pia, Mboneko amewataka wanafunzi katika chuo hicho, kuyatunza majengo hayo, kuimarisha mazingira ya usafiri, pamoja na kusoma kwa bidii, ili waje kuwa Walimu Wazuri na Kufaulisha wanafunzi.

Naye Mkuu wa Chuo hicho cha Ualimu John Nandi, amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kupambana kukikarabati chuo hicho, na kubainisha kuwa kwa sasa kinavutia, na idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 500 hadi 700.

Alisema ujenzi na ukarabati wa Majengo chuoni hapo ulianza mwaka 2016 na umekamilika May mwaka huu, ambapo tayari majengo hayo yameanza kutumiwa na wanafunzi.

Nao baadhi ya wanafunzi chuoni hapo akiwamo Leokadia Cosmas, wameipongeza Serikali kwa kuwaboreshea mazingira mazuri chuoni hapo, huku wakiahidi kuyatunza majengo hayo pamoja na kusoma kwa bidii.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza mara baada ya kumaliza ziara katika chuo cha Ualimu SHYCOM. Picha na Marco Maduhu

Mkuu wa chuo cha Ualimu SHYCOM John Nandi akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwa kupigania chuo hicho hadi kufanyiwa maboresho ya hali ya juu.

Mwanafunzi Leokadia Cosmas akiipongeza Serikali kwa kukifanyia maboresho chuo hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa katika ziara ya kukagua Majengo ya chuo cha Shycom.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea na ukaguzi wa Majengo katika Chuo cha Ualimu SHYCOM.

Ukaguzi ukiendelea.

Ukaguzi ukiendelea.

Muonekano wa madarasa mapya Chuo cha SHYCOM.

Muonekano wa madarasa mapya.

Muonekano wa madarasa mapya.

Ukaguzi bweli la wavulana ukiendelea.

Ukaguzi bweli la wavulana ukiendelea.

Ukaguzi bweli la wavulana ukiendelea na kuwataka wanafunzi wazingatie suala la usafi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akikagua ujenzi wa miundombinu ya choo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akikagua Majiko ya kupikia katika chuo cha SHYCOM.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa kwenye Maktaba ya Vitabu katika chuo cha SHYCOM.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwasihi wanafunzi katika chuo cha SHYCOM wasome kwa bidii, ili waje kuwa Walimu wazuri na Kufaulisha wanafunzi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea kutoa nasaha kwa wanafunzi chuoni hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea kutoa Nasaha kwa wanafunzi chuoni hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea kutoa nasaha kwa wanafunzi chuoni hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho cha Ualimu SHYCOM.

Na Marco Maduhu- Shinyanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...