Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugulile amewataka wanawake wa Kigamboni Kutumia fursa za mikopo ya wakina mama   isiyo na riba ili kujiinua kiuchumi.

Pia amewataka Umoja wa wanawake Kigamboni (UWAKI) kurasimisha umoja wao na kutambulika rasmi.

Akiyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Umoja  wa wanawake Kigambini (UWAKI), Dk Ndugulile  ameutaka umoja huo kuendelea kuwa na mshikamano ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Dk Ndugulile amesema, “umoja na mshikamano ndio chachu ya maendeleo nawasihi kuendelea kujiinua kiuchumi na kufikia malengo mliyojiwekea,”

Akizungumzia miradi inayoendelea kupitia umoja wa UWAKI, Dk Ndugulile ameweza kuwachangia kiasi cha Shiling Milioni Moja (1,000,000)  ili kujazia mfuko wao kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kimaendeleo ndani ya Jimbo la Kigamboni.

Pia, Mbunge huyo amesisitiza kuendelea kushirikiana na Umoja wa wanawake na Kigamboni kupitia ofisi ya mbunge na kuwataka kujiimarisha kiuchumi kwa kutumia mfuko wa serikali wa mikopo kwa wakina mama ambayo haina riba.

“Ipo mikopo kwa ajili ya akina mama  na haina riba kwa hiyo nawasihi wajitokeze kwa wingi kutumia fursa hiyo kujiinua kiuchumi na kushiriki miradi ya kimaendeleo,” amesema Dk Ndugulile.

Akitoa taarifa fupi ya umoja huo, Mwenyekiti wa UWAKI, Pili Misana  amesema Umoja huo umelenga katika kumuinua mwanamke kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Misana amesema, Umoja wao umejipanga kwenye kufanya miradi ya kimaendeleo ikiwmeo Elimu, Afya, michezo , mazingira na ujasiriamali wakilenga wanawake wote wa Kata tisa za Kigamboni.

“Umoja huu ulianza ili kumuinua mwanamke kimaendeleo na kiuchumi, katika sekta ya elimu, afya, michezo na mazingira,” amesema Misana

Aidha, amesema ndani ya umoja huo wameweza kukusanya fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ambapo tayari mradi mmoja upo mbioni kuanza.

Misana amewashukuru wadau mbalimbali wa kimaendeleo walioweza kushirikiana nao katika kufanikisha jambo hili ikiwemo GSM, TRA, CRDB, NMB, Taifa Gas na Clouds City.

Katibu Wa UWAKI, Sharifa Shaban amesema hadi kufikia sasa umoja wao una viti 40 na turubai moja ambalo wanakodisha, ila malengo yao ni kufikisha viti 1,000 na matenti 10 sambamba na mabusati 100.

Mmoja ya wanachama wa UWAKI Farida Mtoto amewashukuru wanawake wa Kigambonj ambao kwa pamoja wameamua kujiunga na kuanzisha kwa umoja huo wenye lengo la kumuinua mwanamke kiuchumi.

Farida amesema, wanazidi kuwakaribisha wanawake wengine wa Kigamboni kuja kujiunga kwa sababu utaratibu ni rahisi na ada ya uachama ni nafuu na inalipwa kila mwezo.

Umoja wa wanawake wa Kigamboni (UWAKI) ulianza rasmi Mwezi June mwaka huu ukiwa na wanachama 30 lakini hadi kufikia Septemba wanachama wameongezeka na kufikia 135 na tayari ukiwa umesajiliwa.

 







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...