Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chemba ya wenye Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA),Dkt Said Mtemi Kingu akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Na mwandishiWetu, Dar es Salaam
KATIKA hatua inayotafusiriwa kuwa ni ya kimaendeleo, Dkt Said Kingu, ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu, amechaguliwa kuwa kuwa mmoja wa wajumbe wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo(TCCIA).

Akizungumzia hatua hiyo hapa jana, Mwenyekiti wa Bodi, Bw Paul Koyi, amesifu uamuzi huo na kusema chemba yao kila mara inajitahidi kutumia ujuzi wa wataalamu mbalimbali ili kuendeleza chemba na jumuiya ya biashara nchini Tanzania.

“Tunautafasiri uamuzi huu kama hatua nzuri katika maendeleo ya chemba yetu. Kila mara tunajitahidi kutumia wataalamu wetu kuendeleza chemba yetu na kuinufaisha jumuiya ya biashara nchini,” amesema Bw Koyi ambaye pia ni Rais wa TCCIA.

Dkt.Kingu amesishukuru jumuiya hiyo kwa kumchagua kuwa mjumbe wa bodi na kusema hiyo ni heshima kubwa kwake.“Nitatumia uwezo wangu na maarifa niliyonayo kutoa mchango stahiki na kuiletea maendeleo chemba yetu na nchi kwa ujumla.” Ameahidi Dkt.Kingu na kuongezea kuwa amejiunga na chemba hiyo kwa sababu ya umuhimu wake katika kujenga uchumi wa nchi.

Ameeleza kuwa siku zote anaamini katika kufanyakazi kwa ushirikiano ndio siri ya mafanikio mahali ppoote na kuongeza kuwa anaamini kuwa mjumbe wa bod hiyo kutaongeza kasi ya utendaji.“Tanzania ni yetu , mimi ni Mtanzania. Ni lazima niitumikie nchi yangu kwa faida ya yangu na nchi kwa ujumla hivyo kuwa kwangu mjumbe wa bodi ya TCCIA ni sehemu ya kuitumikia nchi. Chemba hii inagusa watu wengi katika nyanja tofauti za kiuchumi.” Ameeleza.

Dkt.Kingu ameseama sekta binafsi ina nafasi kubwa katika kukuza uchumi wa nchi kwani inatoa ajira nyingi, na kuwa kupitia biashara imekuwa ikiingiza fedha ya kigeni ambayo inachochea maendeleo.

“Rai yangu kwa wanataaluma wengine nchini wazione taaluma zao kuwa ni biashara hivyo wajiunge ma chemba hii ili waweze kupata fursa za kuendeleza biashara zao,” amesema Dkt.Kingu.

Amesema wapo wataalumu ambao wamefungua ofisi za ushauri. Amewashauri wazione ofisi zao kuwa ni biashara kama biashara nyingine na kwamba wana kila sababu ya kujiunga na TCCIA ili waweze kupata mbinu za kuboresha biashara zao, kukuza vipato vyao na kuchangia katika kukuza uchumi wa Tanzania.

Wajumbe wengine wa bodi ni Bi.Njile Bwana, Bi.Eutropia James, Bi Judith Karangi amabye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA na Katibuwa bodi, Dkt.Meshack Kulwa ambaye ni makamu mwenyekit (biashara), Bw. Swallah S Swallah makamu (kilimo), Bw.Clement Bocco makamu (viwanda) mwenyekiti Bw Koyi a mbaye pia ni Rais wa Chemba hiyo.

Chemba hiyo ilianzishwa mwaka 1988.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...