Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Jumla ya Viwanja 21 viliweza kutumika katika michezo ya Ligi Kuu Kwa msimu wa mwaka 2020/21.

Katika taarifa hiyo, Uwanja wa Benjamin Mkapa uliweza kuingiza mashabiki wengi zaidi na mapato ukilinganisha na viwanja vingine.
 
Timu zimekuwa zikitegemea vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo wadhamini, wafadhili, michango ya wanachama na makusanyo ya viingilio vya uwanjani ili kuendesha timu zao.

Katika orodha iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzanja kupitia Bodi ya Ligi, Uwanja wa Benjamin Mkapa umeshika namba moja kwa kupata mapato makubwa sambamba na mashabiki.

Hii ni orodha ya Viwanja vilivyoingiza mapato


1. Uwanja wa Benjamin Mkapa (Dar es Salaam) – Bilioni 1.9
-

2. Uwanja aa Jamhuri (Dodoma) – Milioni 287.3


3. Uwanja wa Sokoine(Mbeya) – Milioni 227.05
4. Uwanja wa CCM Kirumba (Mwanza)- Milioni 191.9
5. Sheikh Amri Abeid (Arusha)- Milioni 122.7
6. Uwanja wa Jamhuri (Morogoro)- Milioni119.8
7. Uwanja Kambarage (Shinyanga)- Milioni 115.9
8. Uwanja wa Gwambina (Mwanza)- Milioni 114.6
9. Uwanja wa Nelson (Rukwa)- Milioni 80.9
10. Azam Complex-Chamazi (Dar es Salaam)- Milioni 72.99
11.Uwanja wa Karume (Mara)- Milioni 66.4
12.Uwanja wa Mkwakwani (Tanga) -Milioni 65.6
13. Uwanja wa Kaitaba (Kagera)- Milioni 63.2
14. Uwanja wa Majaliwa (Lindi)- 32.4
15. Uwanja wa Uhuru (Dar ) -Milioni 28.3
16. Uwanja wa Highland Estate - Milioni 17.9
17. Uwanja wa Ushirika (Kilimanjaro)- Milioni 10.3
18. Uwanja wa Mabatini (Pwani)- Milioni 8.8
19. Uwanja wa Nyamagana (Mwanza)- Milioni 4.9
20.  Mwadui Complex (Shinyanga)- Milioni 1.9
21. Uwanja wa CCM Gairo (Morogoro)- 195,000

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...