KAMPUNI ya iStore ambao ni wauzaji pekee wa bidhaa za Apple hapa nchini Tanzania, wanajivunia kuzindua Kikundi cha watumiaji wa bidhaa za Apple Tanzania kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook

Kundi maalum kwa watumiaji wa huduma hizo litawapatia watumiaji wake kuwasiliana, kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu bidhaa hizo na kujibiwa, ikiwa ni sehemu ya kuwaleta pamoja na kuwarahisishia kupata huduma kwa haraka. 

Akizungumza katika hafla fupi ya kuzingua kundi hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya iStore Tanzania, Vipul Shah alisema kuwa kuzinduliwa kwa  Kundi hilo kutasaidia kuwaleta pamoja wameteja wao na kuwarahisishia kupata huduma kwa haraka.

“Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya bidhaa za Apple nchini Tanzania hasa simu za iPhone, hivyo kuanzishwa kwa kundi hili kutasaidia kuwaleta pamoja watumiaji wote na wateja wetu kwa ujumla ili kupata huduma kwa harama” alisema Shah.

Aliendelea kusema kuwa “Hivyo nawaasa wale wote ambao sio watumiaji wa huduma zetu waanze sasa kwani kuna kuna faida kubwa sana ukiwa mtumiaji wa bidhaa za Apple”. 

Mratibu wa Usambazaji wa Kampuni ya Redington, Vipul Prajapati (kulia) akimkabidhi tuzo maalum kutoka Kampuni ya Apple, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya iStore Tanzania, Jully Martin katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za iStore, Mikocheni jijini Dar es salaam hivi karibuni. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya iStore Tanzania, Vipul Shah.
Sehemu ya wateja wa iStore na wadau wa kundi la watumiaji wa bidhaa za Apple Tanzania wakiwa kwenye hagla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...