Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa yasiyoambukiza  imeupongeza mkoa wa Rukwa kwa mafanikio iliyoyapata katika kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo mkoa una maambukizi ya asilimia 4.4 chini ya kiwango cha kitaifa cha 4.7

Pongezi hizo zimetolewa  leo (27.09.2021) na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Hassan Toufiq (Mb) wakati wa kikao na viongozi na watumishi wa serikali na wadau mjini Sumbawanga.

Akitoa taarifa ya mkoa ,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu alisema mkoa una watu 34,000 wanaoishi na VVU/UKIMWI ambapo kati yao 28,000 sawa na asilimia 95 wametambuliwa na wanapata huduma za tiba na dawa za kupunguza makali ya VVU

Kuhusu huduma za tohara kwa hiari, Dkt. Kasululu alisema wanaume 34,549 kati ya lengo la watu 35,999 wamepatiwa huduma hiyo kwenye mkoa huo ikiwa ni makakati  wa kupungunza maambuzi ya VVU/Ukimwi.

Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Jaqueline Msongozi (Mb) akizungumza kwenye kikao hicho alitoa rai kwa wanawake kote nchini kutokubali kuwa na mahusiano ya kingono na wananume amabao hawajafanyiwa tohara ili kuondoa hatai ya kupata magonjwa.

" Niwashauri wanawake wenzangu wa Rukwa na kote nchini kabla ya kuwa na mahusiano ni vizuri kujua endapo mwanaume amepata tohara au la .Ukikuta hajapata tohara basi usitoe huduma" alisema Mhe. Msongozi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Denis Bandisa amesema anashukuru kwa waheshimiwa wabunge hao kupata nafasi ya kutembelea mkoa wa Rukwa kujionea hali ya utoaji huduma za afya kwenye masuala ya UKIMWI na magonjwa mengine.

Bandisa ameihakikishia kamati hiyo kuwa maeleokezo na ushauri watakao utoa wakati wa ziara yao ya siku mbili mkoani Rukwa yatafanyiwa kazi na mrejesho utatolewa kwa Bunge.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI,Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa yasioambukiza Mhe. Fatma Hassan Toufiq akiongoza kikao na viongozi na wadau wa mkoa wa Rukwa leo mjini Sumbawanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw. Denis Bandisa akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI leo waliofanya ziara ya kikazi mkoani Rukwa kukagua masuala ya utoaji huduma.

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu akitoa taarifa ya mkoa kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI,Kifua Kikuu na magonjwa yasiyoambukiza leo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge  mjini Sumbawanga.
Waheshimiwa Wabunge na wajumbe wa Kmati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi wakiwa kwenye kikao leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjni Sumbawanga.
Mbunge wa Viti Maalum toka mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquline Msongosi amewashauri wanawake nchini kutokuwa na mahusiano na wanaume ambao hawajafanyiwa tohara ili kuepuka kuambizwa magonjwa ikiwemo VVU/UKIMWI.Ametoa rai hiyo leo mjini Sumbawanga wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI.
Mbunge wa Longido Dkt.Steven Kiruswa  akizungumza kwenye kikao cha wadau na Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI ambapo amepongeza mkoa wa Rukwa kwa kuwa na takwimu nzuri kuhusu hali ya maambukizi ya VVU/UKIMWI pamoja na mikakati ya kudhibiti maambukizi ya kifua kikuu. (Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Mbunge wa Malinyi Mhe. Antipas Mgungusi akichangia wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na wadau wa mkoa wa Rukwa ambapo ameshauri takwimu ziwekwe vizuri zikihusisha umri,jinsia na mahali wanapoaishi ili iwe rahisi kuwatambua ba kuwafikishia huduma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...