Na Jamaly Mussa, DSJ

STAA wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva nchini Tanzania Ali Kiba amepokea tuzo mbili (Gold & Silver) kutoka mtandao wa YouTube unaohusiana na maudhui ya video. 

Ni utaratibu wa mtandao huo kutoa tuzo kwa watu walio na wafuasi wengi (subscribers) na sababu za kufanya hivyo ni kuleta hamasa kwa watumiaji wa mtandao huo.

Ali Kiba amefanikiwa kupata tuzo ya Gold baada ya kufikisha zaidi ya wafuasi (Subscribers) milioni moja katika chaneli yake ya YouTube hivi karibuni kutokana na kuachia nyimbo mfululizo na hivyo kumfanya kufikisha wafuasi hao kwa kutembelea chaneli yake hio.

Sababu nyingine inatajwa kuwa ni kutokana na ukubwa alionao katika tasnia hiyo ya Bongo Fleva.

King Kibakupitia ukurasa wake wa Instagram  ameweka video fupi pamoja na picha akionyesha tuzo hiyo ya Gold na tuzo ya Silver kwa kufikisha wafuasi 500,000 katika chaneli yake ya kings Music Records ikionyesha nyimbo za kundi akiwa na staa wenzake wakina Abduilkiba, K2GA na Tommy fleva.

Ali Kiba kwa sasa anatamba katika  kibao ambacho ameshirikiana na Mkali wa muziki Maud Elka kutokea nchini Ufaransa.Kibao hicho kinaitwa  Songi Songi Remix iliyotoka mwishoni mwa Agosti mwaka huu.

Haya hivyo ukiachana na hiyo kazi hiyo Ali Kiba alitoa ngoma ya Salute aliyomshirikisha Rude wa chini Nigeria.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...