Na Karama Kenyunko, Michuzi tv
MAHAKAMA Kuu kitengo cha  Makosa ya Uhujumu Uchumi na  Rushwa maarufu  'Mafisadi' imetoa ufafanuzi sababu za kuzuia idadi kubwa ya watu kuingia katika ukumbi wa wazi  wa mahakama hiyo kusikiliza kesi ya tuhuma za ugaidi  inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA)Freeman Mbowe na wenzake watatu

Akizungumza mbele ya waandishi leo Septemba 16, 2021 Msajili Msaidizi wa Mahakama hiyo Magdalena  Ntando amesema wameweka utaratibu wa watu kutoingia na simu na pia kungia wachache kutokana na sababu za kiafya ikiwa ni pamoja na hali ya maambukizi ya Covid 19 iliyopo nchini sasa.

Amesema, hakuna ruhusa kwa mtu yoyote kutumia simu mahakamani, lakini watu wamekuwa wakiingia na simu mahakamani bila kuzizima,  hivyo kusababisha kelele mahakamani huku wengine wakirekodi mwenendo wa kesi na kutuma mitandaoni kitu ambacho kisheria hakiruhusiwi.

Hivyo amewataka wote wanaoingia mahakamani ama kuziacha nje simu zao au kuzizima kabisa ili kudhibiti kelele mahakamani na kukosekana kwa utaratibu wa kurekodi mwenedo wa kesi.Pia amesema watu waliipokea kwa sura tofauti lakini wanashukuru wamewaelewa.

Amefafanua jukumu la kuchambua ushahidi ni la mahakama na wala siyo la mtu mwingine, hivyo kitendo cha kurekodi mwenedo wa kesi na kurusha kwenye mitandao ya kijamii kunawafanya watu watoe hukumu hata kabla haijafikia wakati wake, amesema

Aidha amesema miundombinu ya ya ukumbi huo wa Mahakama ni watu wachache tu ndio wanaweza kuingia kwani ukumbi unauwezo wa kuchukua watu 45 tu.Wanachukua tahadhari zote kujikinga na ugonjwa wa Covid 19, kwani ni muhimu kwa kiafya watu kujazana ni hatarishi.

"Kwa kawaida tungependa kila mtu ashiriki kusikiliza kesi hii lakini kiafya ni hatarishi lakini pia miundombinu ya ukumbi hairuhusu ndio maana tukaone tupate wawakilishi kwa kila sekta yaani ndugu wa washitakiwa wote, waandishi wa habari na mawakili ambao wao ndio wenye kesi yao," amesema Ntando.

Amesema wametoa nafasi kwa wahusika wenyewe kupendekeza nani aingie na nani asiingie jambo ambalo mwanzoni lilikuwa gumu sana kutekelezeka lakini baadae walielewa na kulitimiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...