Na Karama Kenyunko Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya Uchochezi baada ya Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) kuifuta kesi hiyo.


Hatua hiyo imekuja kufuatia DPP kuwasilisha Nolle mahakamani hapo ya kuonesha kuwa Jamuhuri haina nia ya kuendelea na mashtama dhidi washtakiwa hao.

Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio.


Mbali na Lissu, washtakiwa wengine ni, Wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob.

Mapema wakili wa Serikali Sofia Mzava alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Lwambano kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini DPP amewasilisha hati mahakamani hapo (Nolle Prosequ) chini ya kifungu cha 91 (1) cha CPA kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Katika kesi ya msingi Lissu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa kati ya  Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13, 2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...