WANACHAMA na Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamesogezewa huduma za Mfuko kwa kutumia simu ya kiganjani na wanachotakiwa kufanya ni kujiunga na Mfumo wa PSSSF Kiganjani na PSSSF Popote Mtandao,  Meneja wa Mfuko huo Mkoani Geita Bw. Geofrey Kolongo amewaambia waandishi wa habari.

Akizungumza kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA eneo la Bombambili Mkoani Geita Septemba 23, 2021, Bw. Kolongo alisema Mfumo huo sio tu unarahisisha upatikanaji wa huduma lakini pia  unaokoa muda na kupunguza gharama.

“ Mwanachama akijiunga na mfumo huu halazimiki kutembelea ofisi zetu kupata huduma, badala yake atapata huduma za Mfuko akiwa kwenye shughuli zake au nyumbani,” alisema.

Akifafanua zaidi kuhusu Mfumo huo, Bw. Kolongo alisema ili kutumia Mfumo wa PSSSF Kiganjani Mwanachama atajisajili ili kupata akaunti ya mtumiaji, kisha ataweza kuona michango na taarifa zake za msingi za mwanachama na kwa Mstaafu ataweza kuona taarifa zake za msingi ikiwa ni pamoja na kuona kumbukumbu za malipo ya pensheni ya kila mwezi.

Kuhusu PSSSF Ulipo Mtandao, Bw. Kolongo alisema Mfumo huo unajumuisha Madirisha (Portals) Matatu moja la Mwanachama (Member Portal) linalomuwezesha kuangalia taarifa zake za msingi za uanachama kuangalia Taarifa zake za Michango na kuwasilisha Maulizo mbalimbali kuhusiana na Michango au Uanachama na lolote linalohusiana na Mfuko.

Akieleza zidi Meneja huyo alitaja Dirisha la Pili ni la Muajiri (Employer Portal) ambaye anaweza kuangalia taarifa zake za michango, kuangalia taarifa za madai yahusuyo Taasisi yake yaliyowasilishwa, na anaweza kuwasilisha maulizo ya aina yoyote na Dirisha la Tatu ni dirisha la Malipo (Billing System/Portal) Mfumo huu hutumika kwa ajili ya ukusanyaji wa michango na umeunganishwa na mifumo ya ndani na ule wa malipo ya Serikali, Mfumo utamuwezesha mwajiri kupata control namba inayotumika kwa malipo ya Serikali na anaweza kupata risiti na kuiprinti.

Maonesho hayo yanayoandaliwa kila mwaka na uongozi wa Mkoa wa Geita yalianza Septemba 16 na kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Septemba 22, 2021 na yamebeba kauli mbiu isemayo “ Sekta ya Madini kwa Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu.”

Mfanyakazi wa  Mfuko Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mkoani Geita (Katikati) akiwahudumia Wanachama waliotembeela banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA eneo la Bombambili Mkoani Geita Septemba 23, 2021
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Martha Mkupasi (kushoto) akipata huduma kwenye banda la PSSSF Septemba 23, 2021.
Bw. Geofrey Kolongo, Meneja wa PSSSF Mkoani Geita






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...