KAMPUNIKampuni maarufu ya kubashiri matokeo ya Meridianbet imetoa vifaa vya michezo kwa timu zote zilizoshiriki bonanza la soka la timu za mtaani lililopewa jina la Meridian soccer street bonanza lililofanyika leo kwenye viwanja vya Fire, Dar es Salaam.

Afisa masoko wa Meridianbet, Twaha Ibrahim amezikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni seti za jezi na mipira timu za Kigambo Fc ambayo ilikuwa bingwa, Pemaco Fc ya Mbezi Beach iliyokamata nafasi ya pili, Northern Boyz ya Mbagara na Matombo FC ya Upanga na kubainisha moja ya mkakati wa kampuni hiyo hiyo ni kusapoti timu za mtaani ambazo baadhi ya wachezaji wake ni wateja wao.

Twaha ambaye aliambatana na viongozi wengine waandamizi wa Meridianbet amesema hamasa iliyoonekana kwenye bonanza la leo limethibitisha namna vijana wengi wana vipaji lakini hawapati nafasi ya kuonekana.

Katika bonanza hilo, Kigamboni FC ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Pemaco mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliokuwa na amsha amsha kwa mashabiki wa pande zote mbili.

Babi Nyanda ndiye alikuwa shujaa wa Kigamboni baada ya kufunga mabao mawili pekee na jingine likifungwa na Salum Chubi na timu hiyo kuondoka na seti ya jezi na mipira miwili huku Gerald Gerald 'Samatta' na Baina Juma wakifunga yale ya Pemaco na kumaliza wa pili wakiondoka na seti ya jezi na mpira mmoja.

Northern Boys walimaliza wa tatu na kuzawadiwa seti ya jezi na Matombo FC walimaliza wa nne na kupewa mipira mitatu.

Enock Babi wa Kigamboni FC alikuwa mfungaji bora wa bonanza hilo.

Twaha amesema Babi atawekewa kitita cha Sh 30,000 hadi 50,000 kwenye akaunti yake ya Meridianbet ambayo ataitumia kubashiri matokeo ili kujishindia mamilioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...