MGONGANO wa kimaslahi baina ya mawakili wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake, mawakili hao wameomba kila Mshtakiwa kuwa na uwakilishi wake mahakamani hapo

Hali hiyo imeibua hoja za kisheria kutoka Upande wa Mashitaka, Utetezi na Mahakama yenyewe kuhusu  kuepusha muingiliano wa maelezo ya shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri, Ramadhan Kingai dhidi ya mshitakiwa wa Pili, Adam Kasekwa.

Kutokana na mgongano huo Jaji Mustafa Siyani anayesikiliza kesi hiyo ameeleza jambo hilo linaleta tafakari kubwa, na sio la kwenda nalo haraka kwani kwa kufanya hivyo huenda kukaleta athari baadaye ambapo.
 
"Ninahitaji muda kidogo kutafakari jambo hili kabla ya kulitolea maamuzi, hivyo baada ya dakika 15, nitatoa uamuzi,"amesema Jaji Mustapha Siyani

Katika uwakilishi huo, Mbowe anawakilishwa na Jopo la Mawakili takribani 12 akiwemo Wakili Kibatala mwenyewe, Kasekwa  anawakilishwa na Wakili John Mallya huku Wakili Nashon Nkungu na Jeremiah Ntobesya wakimwakilisha mshtakiwa Bwire  na Lingwenya anawakilishwa na Dickson Matata.

Mbali ya Mbowe na Kusekwa, washitakiwa wengine ni Mohammed Lingwenya, Ramadhan Bwire.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...