Na John Walter,Manyara .

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ametembelea kiwanda cha Mati Super Brands Limited kinachozalisha vinywaji vikali kilichopo wilayani babati na kujionea shughuli mbalimbali zikiendelea ambapo amepongeza juhudi zinazofanywa na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho David Mulokozi katika kuongeza uzalishaji na kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi wa Mji wa Babati na Manyara kwa ujumla.

Aidha ameipongeza kiwanda hicho kwa kulipa kodi ya wastani wa shilingi milioni 400 kwa kila mwezi hivyo kuwa moja kati ya walipa kodi wakubwa katika wilaya ya Babati na Mkoa wa Manyara kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Kiwanda hicho David Mulokozi amepongeza ziara ya Mkuu wa Mkoa katika kiwanda hicho kwani ni mdau mkubwa wa maendeleo katika Mkoa huo na amekua kiungo muhimu katika kuhamasisha maendeleo katika Mkoa wa Manyara.

Aidha amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kulipa kodi kwa uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kusukuma maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

“Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa viwanda hivyo kulipa kodi ni jukumu la msingi tulilonalo kama wawekezaji” Anaeleza David Mulokozi Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Mati Super Brands Limited

Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Gwandumi Mpoma alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora na zinazokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Gwandumi alisema kuwa suala la ubora wa bidhaa ;limekua likizingatiwa tangu kiwanda hicho klinaanzisha hivyo kupelekea bidhaa hizo kufanya vizuri sokoni.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara akiangalia Uzalishaji ukiendelea katika Kiwanda cha Mati Super Brands Limited.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited David Mulokozi(kushoto) akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited David Mulokozi(kushoto) akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...