Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewataka Wakuruguenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kwamba Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wanapewa muda mrefu wa kuhudumu kwenye nafasi hiyo na siyo kuwabadilisha mara kwa mara ili kutopoteza muedelezo wa usimamizi makini wa Mfuko huo ambao lengo lake ni kuzinyanyua kaya maskini.

Kauli hiyo imetolewa leo Mkoani Kilimanjaro na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deo Ndejembi alipokua akizungumza na waratibu wa TASAF Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Wilaya zake zote ambapo amesisitiza kuwa ni vema Wakurugenzi kuwapa muda wa kutosha waratibu wa Mfuko huo ili waweze kufanya kazi zao kwa kipindi kirefu jambo ambalo litachangia kuwepo kwa muendelezo wa huduma zinazotolewa na TASAF.

Ndejembi pia amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha kuwa waratibu wa TASAF wa kila Halmashauri wanaingia kwenye vikao vya kila wiki vya Wakuu wa Idara za Halmashauri huku pia akiwataka kujadili hoja za TASAF kwenye vikao hivyo kwani itasaidia kuinua uelewa wa Mfuko huo na kufahamu nini ambacho kinaendelea kwenye maeneo yao.

"Tutawaandikia na wenzetu wa Tamisemi ili kuweza kupata uelewa wa pamoja kwani nafahamu yapo makubaliano yaliyosainiwa ya pamoja kati ya TASAF na Tamisemi ambacho kipengele cha kuwataka waratibu wa TASAF kuingia kwenye vikao vya kila wiki vya wakuu wa Idara kwenye Halmashauri sasa Wakurugenzi walisikie hili waratibu waingie kwenye vikao hivyo na hoja za TASAF zipewe kipaumbele.

Suala la waratibu kupewa muda wa kuhudumu nafasi hizi ni la msingi kwani linachangia kuongeza muendelezo wa mradi wa TASAF, ambapo mradi huu ni mradi mkubwa wa Serikali ambao unagusa maisha ya mamilioni ya Watanzania ambao wanaguswa moja kwa moja na mkono wa Serikali, tusiwabadilishe mara kwa mara," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Ndejembi amesisitiza Wakurugenzi hao wa Halmashauri kuhakikisha kuwa waratibu wa TASAF wanafanya kazi zao za TASAF huku pia akiwataka waratibu hao kuongeza Ubunifu katika kazi Ili kuweza kufikia kaya nyingi zaidi.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi (katikati) akiwa Katika picha ya pamoja na Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza kufanya nao mazungumzo.

Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi alipokutana na kuzungumza nao leo Mkoani humo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi akisisitiza jambo kwenye kikao chake cha pamoja na Waratibu wa TASAF Mkoa wa Kilimanjaro alipokutana na kufanya nao mazungumzo leo.


Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi alipokutana na kuzungumza nao leo Mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...