Kampuni
ya kiutafiti ya Reputation Poll International LLC, imemtaja Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kuwa miongoni mwa
watendaji wakuu 50 wenye sifa nzuri kiutendaji barani Afrika kwa mwaka
huu wa 2021.
Nsekela
amefanikiwa kuwa mmoja wa watendaji wakuu wa benki barani Afrika
walioonyesha weledi katika sekta ya uwekezaji na uvumbuzi wa
kiteknolojia katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na janga la
Covid-19.
Kampuni
hiyo ya Reputation Poll International LLC, imesema iliona umuhimu wa
kuwatambua viongozi katika sekta ya kibenki kwa kutambua mchango wa
sekta hiyo katika jamii, kuunganisha watu na biashara pamoja na uchumi
kiujumla kwa njia moja au nyingine.
Utafiti
huo unaofanywa kila mwaka, uliweza kuangalia pia mchango wa watendaji
wakuu wa mabenki 50 barani Afrika kwa kuangalia jinsi gani waliochochea
au kupitia nafasi zao kufanya mapinduzi ya kisekta katika maeneo
yafuatayo; ubora, Uadilifu, Uaminifu, Utaalam, Teknolojia, na urahisi wa
upatikanaji wa mikopo.
“Wale waliosaidia mabenki yao kufikia mafanikio makubwa zaidi,” kampuni hiyo imesema.
Jina
la Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Nsekela lilikua la kwanza
katika orodha ya watendaji wakuu Afrika, na ni Mtanzania pekee
aliyeorodheshwa na kampuni hiyo.
Hata
hivyo hii ni mara ya pili kwa Nsekela kutambulika kimataifa kupitia
uongozi wake, baada ya mwaka jana 2020 kutajwa katika jukwaa la viongozi
bora na jarida la African Ledership Magazine.
Katika
taarifa yao kampuni ya Reputation Poll International LLC imesema sekta
ya kibenki iliathirika kwa kiasi kikubwa na janga la Covid-19 duniani,
hasa kwa nchi za Kiafrika na hivyo kupelekea faida kwenye mitaji au
kupungua hadi kufikia asilimia 7 mwaka 2020 kutoka asilimia 14 mwaka
2019 (McKinsley,2021).
Hata
hivyo chini ya Nsekela Benki ya CRDB iliendelea kutengenza faida mwaka
hadi mwaka. Tangu alipojiunga na benki hiyo mwaka 2018 kama mtendaji
mkuu, Benki ya CRDB imekuwa ikiwekeza kwa kiasi kikubwa katika mifumo ya
kidijitali, ikiwa ni moja ya vitu vilivochangia ukuaji wa faida kwa
zaidi ya asilimia 87 mwaka 2019 na kufikia Sh120 bilioni kutoka Sh64.2
bilioni zilizopatikana kama faida mwaka 2018.
Katika
miaka yake mitatu ndani ya benki hiyo, utendaji wa Benki ya CRDB
umeimarika ukichochewa na mageuzi ya kimkakati. Mwaka jana benki hiyo
ilivunja rekodi kwa kuongeza faida yake kwa asilimia 35 na kufikia Sh236
bilioni kutoka Sh175 bilioni za mwaka 2019. Na katika matokeo ya fedha
ya nusu ya mwaka huu wa 2021 benki iliweza kuongeza faida yake kwa
asilimia 26 kufikia Sh88.6 bilioni ukilinganisha na Sh70.4 bilioni
zilizopatikana nusu ya mwaka jana 2020.
Akizungumza
baada ya kuchapishwa kwa orodha hiyo Nsekela alisema ni jambo jema kuwa
miongoni mwa viongozi wenye utendaji bora Afrika na akasema mafanikio
hayo yamechangiwa na wateja, wadau na wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Nsekela
amesema licha ya changamoto zilizoletwa na janga la Covid-19, Benki ya
CRDB imeendelea kupata matokeo mazuri ya kifedha kutokana na ukuaji
mzuri wa mapato na faida.
“Pamoja
na changamoto tulizokumbana nazo tumeweza kuboresha biashara yetu kwa
kuweka mikakati madhubuti ya mabadiliko na kuchukua hatua kwa wakati,”
amesema.
Uwekezaji
thabiti katika mifumo ya kidijitali umewezesha zaidi ya asilimia 80 ya
miamala kufanywa nje ya matawi ya benki nchini kote kwa hivyo kuongeza
ujumuishaji kifedha kulingana na ajenda ya serikali.
“Tumeongeza
kasi ya miradi ya kujipambanua kidijitali ili kuhakikisha kuwa
tunahudumia wateja wetu kwa ufanisi wakati pia tukizingatia miongozo ya
afya, ” Nsekela amesema.
Ameongeza,
"Lengo letu ni kuendesha matumizi ya njia zetu za dijitali kama
SimBanking, Internet banking na CRDB Wakala, ambazo itapunguza umuhimu
wa wateja wetu kutembelea matawi.”
Chini
ya Nsekela Benki ya CRDB imeweza kukuza biashara yake kwa kiasi kikubwa
kwa kufanya uwezeshaji mkubwa kwa sekta binafsi. Benki hiyo pia imekuwa
mstari wa mbele kusaidia serikali kutekeleza miradi ya kimkakati, kama
vile mradi wa reli ya kisasa Standard Gauge Railway pamoja na mradi wa
kufua umeme wa Nyerere Hydro-electric Power Project.
Tangu
Oktoba 2018, wakati Nsekela alipoingia Benki yay a CRDB, benki hiyo pia
imeongeza uwekezaji katika kusaida jamii kupitia miradi kama mbio za
CRDB Bank Marathon ambayo mwaka huu zilikusanya nusu bilioni kutumiwa
katika matibabu ya watoto katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete
jijini Dar es Salaam na ujenzi wa kituo cha kisasa cha kupiga simu cha
Ocean Road Cancer institute, na kampeni ya ‘Pendezesha Tanzania’
iliyozinduliwa katikati ya mwaka jana ikiwa na mpango wa kupanda miti
milioni moja na nusu nchini kote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...