Na John Walter-Manyara

Jumla ya wahamiaji haramu 44 kutoka Ethiopia wamekamatwa wilayani Babati mkoani Manyara wakiwa katika harakati za kwenda nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ijumaa Septemba 17,2021,mjini Babati kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa jeshi la Polisi Marrison Mwakyoma, alisema wahamiaji hao walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya fuso yenye namba za usajili T 565 CEZ iliyokuwa inaendeshwa na dereva aliejitambulisha kwa jina la ambapo polisi waliisimamisha gari hilo eneo la kizuizi cha Magari Minjingu.

Kamanda amesema polisi walivyomuhoji Dereva alidai anakwenda Iringa kufuata samaki huku akikataa kufungua gari akidai friji litayeyusha barafu na kwamba hadi wafike eneo la samaki ndipo wangelifungua gari hilo.

“Lakini polisi wakasema no,na baada ya kulazimishwa sana na wale kuendelea kubembeleza na kuomba kutoa chochote ili waruhusiwe kupita, askari wakastuka na kuamua kufungua kwa lazima na kuwakuta raia hao wakiwa wamebanana katika gari hiyo” alisema Mwakyoma.

Amesema wahamiaji hao wataendelea kuwahoji wakishirikiana na idara ya uhamiaji na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Pia Kamanda Mwakyoma amesema siku chache zilizopita waliwakamata wahamiaji haramu 2 raia wa Ethiopia waliosimamisha gari na kuomba lifti wakitokea wilaya ya Monduli.

Hata hivyo aliwataka watu wanaojihusisha na biashara ya kusafirisha wahamiaji hao waache mara moja kwa kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na uhamiaji hawatawavumilia.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...