NA MWANDISHI WETU, GEITA

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema utayatumia Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita kutoa elimu na kuwahudumia wanachama wake na wananchi kwa ujumla.

Maonesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo “ Sekta ya Madini kwa Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu,”  yameanza Septemba 16, 2021 kwenye eneo la EPZ lililoko Bombambili Mkoani humo na yatafikia kilelele Septemba 26.

Akizungumzia ushiriki wa Mfuko kwenye Maonesho hayo, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita, Bw. Geofrey Kolongo, alisema Maonesho hayo ambayo huandaliwa na Mkoa na kufanyika kila mwaka ni fursa nzuri kwa Mfuko kukutana na wanachama wake na wananchi kwa ujumla ili kutoa huduma na elimu kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii.

Alisema Wanachama wa PSSSF ni watumishi wote wa Umma na watumishi wote wa Mashirika na Taasisi ambazo Serikali ina Hisa zaidi ya Asilimia 30.

“Kwa muktadha huo, utaona wanachama wetu wengi wako hapa na tumejipanga kutoa elimu kuhusu Mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko ikiwemo Pensheni za kila mwezi, Fao la uzazi, Fao la kukosa Ajira, Taarifa kuhusu Michango ya mwanachama, Mstaafu anaweza kuhakiki taarifa zake, Taarifa kuhusu uwekezaji lakini pia kuna huduma nyingine ya kidigitali, PSSSF Kinganjani na PSSSF ulipo mtandaoni .” Alifafanua Bw.Kolongo.

Akieleza zaidi alisema, Mwanacham au mwananchi mwingine yoyote akifika kwenye banda letu atahudumiwa kama ambavyo anavyohudumiwa kwenye ofisi zetu za PSSSF zilizosambaa nchi nzima Bara na Visiwani.

Mfuko wa PSSSF ulianza Tarehe 1 Agosti, 2018 baada ya Serikali kuunganisha Mifumo Minne ya PPF,PSPF, LAPF na GEPF.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mkoa wa  Geita, Bw. Geofrey Kolongo (kulia), akimhudumia mwanachama alietembelea banda ya PSSSF katika maonesho ya Teknilojia ya Madini eneo la Bomba Mbili viwanja vya EPZA Mkoani hum oleo Septemba 17, 2021.

Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu akipata maelezo KUTOKA kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba wakati alitutembelea Banda la Mfuko huo leo  Septemba 17, 2021.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mkoa wa  Geita, Bw. Geofrey Kolongo (kulia), akizungumzia huduma mbalimbali zitolewazo na PSSSF kwenye maonesho hayo. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...