Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ahani msiba wa Bi Rose Mrema(Mke wa Mzee wa Agustino Lyatonga Mrema) aliyefariki jana saa 8 Mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Maziko yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 21/9 Nyumbani kwake kijiji cha Kiraracha-Vunjo Mkoa wa Kilimanjaro,Kwa niaba ya Serikali Mhe.Rc Makalla ametoa salamu za Rambirambi za pole kutoka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,pia salamu za pole kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambao wote wametoa pole kwa Familia ya Mzee Agustino Lyatonga Mrema kwa Kumpoteza mwana Familia,Mama katika Familia.
Bwana Ametoa ,Bwana Ametwaa Jina lake Lihidiwe. 






Apumzike kwa Amani Bi Rose Agustino Lyatonga Mrema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...