- Ni Kufuatia Wizi huo kuibuka upya kwenye baadhi ya maeneo.

- Vibaka wanaosumbua mtaani kukiona.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuanza msako wa kuwabaini na kuwakamata Wezi wa Vifaa vya Magari  Na vibaka na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Kikao Cha tathimini ya ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo kwa Jimbo ambapo amesema kumeanza kuibuka vitendo vya Wizi na kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo hawezi kulifumbia macho.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na kuwakanya ili wasijekuingia kwenye mikono ya Vyombo vya dola.

Agizo hilo limetolewa kwa mikono miwili na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Muliro Jumanne ambae amewaelekeza makamanda wote wa Mikoa ya kipolisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu Mara moja.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...