Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

SEPTEMBA 25, 2021 ni siku ambayo imepangwa kufanyika Usiku wa Kihistoria uliopewa jina la Usiku wa Ruvu Shooting, mahsusi kutambulisha Wachezaji wa timu hiyo, uzinduzi wa Jezi zitakazotumika msimu ujao tukio likienda sambamba na Wasanii kedekede kutumbuiza katika usiku huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire amesema kuwa malengo ya msimu huu wa mashindano ni kuleta ushindani mkubwa na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, amesema endapo watakosa Ubingwa huo watahakikisha wanashiriki na kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Masau ameeleza kuwa Mgeni rasmi katika siku hiyo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abuubakar Kunenge, ambapo usiku huo utakuwa tofauti na timu nyingine za Soka hapa nchini zinazofanya matamasha yake kabla ya msimu wa mashindano kuanza.

Masau amesema kuelekea siku hiyo ya Septemba 25, timu hiyo itafanya shughuli mbalimbali katika Jamii hususani eneo la Kibaha, Mlandizi ambapo timu hiyo inapatikana. “Wenyeji wa Kibaha, Mlandizi wenye timu yao watakuwa pamoja nasi kuzungumzia malengo yetu kuelekea msimu ujao ikiwa lengo kubwa ni kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara”.

Wasanii wa Bongo Fleva na Hip Hop walitajwa kutumbuiza siku hiyo ni Aslay, Dully Sykes, Tunda Man, Nick Mbishi, Dullah Makabila pamoja na Bendi ya Jeshi (832 KJ - Ruvu JKT) iliyotunga wimbo maalum kwa ajili ya timu hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...