Na Amiri Kilagalila,Njombe

Serikali kupitia wakala wa vipimo mkoani Njombe imesema kuwa ipo mbioni kuanzisha mchakato wa kuwa na kipimo kimoja kitakachotumika kupimia mazao mbalimbali ya kilimo ili kuepusha hasara ambazo amekuwa akizipata mkulima kwa miaka mingi.

Akizungumza katika mafunzo maalumu ya wakulima yanayohusu masauala ya vipimo Mkurugenzi wa huduma za biashara kutoka wakala wa vipimo makao makuu Deogratius Maneno amesema kuwa hivi sasa serikali imeanza mchakato huo kwa kuunganisha wizara tatu,wizara ya kilimo,wizara ya viwanda na biashara pamoja na wizara ya tamisemi ili kuleta suruhu ya pamoja kuhusu changamoto ya .

“Tumepokea maoni ya watu wengi na bado yanaendelea kutolewa na sisi tunawashauri tupime ingawa serikali kupitia wizara tatu baada ya kupata maoni ya watu mbali mbali kwenye maswala haya la Lumbesa tuje na tuje na msimamo wa nchi nzima”alisema Maneno

wabunge wa mkoa wa Njombe akiwemo Dr Pindi Chana mbunge viti maalumu Njombe pamoja Deo Mwanyika mbunge wa Njombe mjini wamesema.

“Mfumo wa biashara unaweza ukatufanya tusiwe matajiri kama tunavyotaka na ndio maana wataalamu wapo hapa leo kutusaidia kujua kuwa hii Lumbesa ina dawa”alisema Mwanyika

Naye Pindi Chana alisema “Mafunzo haya yatatusaidia sana na kimsingi wananchi wa Njombe zaidi ya asilimia 60 ni wakulima lakini swala la vipimo limeendelea kuwa changamoto na wakulima wanalaliwa sana”alisema Pindi Chana

Mkuu wa mkoa wa Njombe Injinia Marwa Rubirya ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo amesema upo umuhimu mkubwa wa vipimo kwa wakulima.

“Moja ya msisitizo mkubwa ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na vipimo sahihi ambavyo vinaleta usawa kwa mkulima na mfanyabiashara kila mmoja kwaeneo lake na tukiwa na vipimo sahihi vitatusaidia serikali kupata takwimu sahihi ya kiasi cha mazao ambayo tunayauza”Alisema Rubirya.


Moja ya kipimo kilichokuwa kikitumika katika mafunzo kwenye semina mkoani Njombe


Mkurugenzi wa huduma za biashara kutoka wakala wa vipimo makao makuu Deogratius Maneno,akieleza malengo ya serikali kuimarisha swalala vipimo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...