Na Mwandishi wetu, Geita

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limesema kuwa kuwepo kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Metals Refinery Limited (MPMR) kilichopo Jijini Mwanza kumeleta faida kubwa katika Taifa ikiwemo kupatikana kwa ajira kwa watanzania

Hayo yamesemwa na Mhandisi Uzalishajishaji wa Kiwanda hicho mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi aliyetembelea Banda la STAMICO akimuwakilisha Mkuu wa Mka wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel kwenye Maonesho ya Sekta ya Madini yanayoendelea katika uwanja wa Bombambili MjiniGeita.

Ameeleza kuwa Kiwanda hicho kilichopo katika Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza kina uwezo wa kusafisha dhahabu kwa 99.99%  na kwamba zaidi ya watu 100 wamepata ajira kwenye kiwanda hicho.

"Uwepo wa Kiwanda hiki kimeleta faida nyingi ikiwemo Ajira, Teknolojia Mpya kimekuwa na Fursa kwa makampuni ya ndani kuweza kutoa huduma za uzabuni Kiwandani haapo, pamoja na Wilaya husika kupata tozo mbalimbali kutoka katika kiwanda hicho,"amesema.

Kwa upande wake Ofisa Rasilimali watu wa Kampuni ya uchimbaji wa dhahabu iliyopo Biharamuro (STAMIGOLD Biharamuro) Muhunda Nyakiroto ameelezea shughuli za uchimbaji na usalama ikiwemo kutoa elimu ya usalama migodini sambamba na kushiriki katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule na wageni alioambata nao Meneja Masoko na Uhusiano wa STAMICO Geofrey Meena amesema  katika maonesho hayo wamejikita kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shuguli zinazofanywa na Shirika lao pamoja na bidhaa wanazozalisha ikiwemo mkaa mbadala wa makaa ya mawe ambao utatumika kwa matumizi ya nyumbani.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...