KUKUZA SEKTA SANAA, UTAMADUNI...WAJA NA BONGO OPERA

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UBALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania kupitia Kituo chake cha Utamaduni cha Alliance Francaise umesema utandelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta ya sanaa na utamaduni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Alliance Francaise jijini Dar es Salaam Flora Valleur wakati akielezea juhudi za kituo hicho katika kufanikisha maonesho ya sanaa ya maigizo ya Bongo Opera(maigizo ya jukwaani) yanayotarajiwa kufanywa na Lumumba Theatre Group kwa kushrikiana na Kisiwa cha Mayotte.

Kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Lumumba Theatre Group wameanza kuonesha aina hiyo mpya ya sanaa ya majukwaani ambapo Septamba 14 wapo jijini Arusha, Septemba 17 watakuwa jijini Dar es Salaam na Oktoba 7 watakuwa kisiwa cha Mayotte.

"Kituo cha Alliance Francaise ni mtandao wa utamaduni ulianzishwa mwaka mwaka 1883, ni mdau mkubwa wa diplomasia ya utamaduni wa Ufaransa.Kituo hiki kina kazi kubwa mbili, moja ni kukuza lugha ya kifaransa na utamaduni wa lugha ya Kifaransa, mtandao umekuwa mkubwa, unaongoza duniani na uko katika nchi 135.

"Nchi Tanzania mtandao huu ulianzishwa mwaka 1961 jijini Dar es Salaam na baadae Arusha na Zanzibar, zamira dar, arusha na zanzibar, zamira kuu mbili kufundisha lugha ya Kifaransa, tunafundisha lugha ya kifaransa kupitia walimu wetu na mafunzo yataanza hivi karibuni.Kila Jumatano tutakuwa na maonesho ya sanaa na utamaduni, tutakuwa na wanamuziki mbalimbali, mikutano ya wasanii kutoka nchini za Afrika Mashariki,amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Lumumba Theatre Group Dyuto Komba ameushukuru ubalozi wa Ufaransa nchini kwa kuwa sehemu ya kufanikisha Bongo Opera huku akifafanua anaamini watafanya vizuri."Kundi letu lina muda mrefu tangu kundi letu lilipoanza, tumefanya kazi mbalimbali ndani na nje ya nchi , leo tupo na watu wa Mayotte , kwanza niishukuru Serikali  kupitia BASATA kutupa hii kazi,tunashirikiana na Mayotte.

"Pia katika Bongo Opera kutakuwa na watu wa Kenya, tuna msanii pekee Aneth naye atakuwepo katika huu ushirikiano, kitu kikubwa kwanza tutaitangaza nchi,kupitia Bongo Opera tutatangaza mila,desturi, utamaduni wetu na vivutio vyetu,"amesema.

Ameongeza kwamba Bongo Opera  kwao wao  ni ngeni lakini watajifunza kutoka kwa wenzao wa Mayotte, wanajifunza kutoka Kenya, wanajifunza kutoka kwa wenzao wa Mozambiq."Na wao wanajifuza kutoka kwetu, hivyo tunategemea tutafanya vizuri."Septemba 17 tunakuwa na onesho la Bongo Opera jijini Dar es Salaam,tunatarajia Mungu ikimpendeza Oktoba 7 tutakwenda Mayotte na tutakaa huko kama wiki, tukiwa huko tutapeperusha bendera ya nchi yetu.

"Pia tunaushukuru Ubalozi wa Ufaransa kwani mwaka 2017 ulitupeleka katika nchi yao na  tulikaa miezi miwili, hivyo Lumumba tutafanya vizuri kwani sasa hivi tuna uzoefu wa kufanya kazi na mataifa tofauti, "amesema na kuongeza kwenye Bongo Opera pia watakuwa na msanii wa sanaa ya maigizo Mamito Unice Njokii kutoka  Xarata ya Samba nchini Kenya.

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Alliance Francaise jijini Dar es Salaam Flora Valleur akizungumza kuhusu namna ambavyo Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania unashiriki kikamilifu kuendeleza sekta ya sanaa na utamaduni .
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Barazaa Sanaa Tanzania( BASATA)  Matiko Mniko wa pili kulia akizungumzia maigizo ya Bongo Opera wakati wadau wa Sanaa na utamaduni walipokutana Kituo cha Umaduni cha Alliance Francaise kwa ajili ya kujadili maonesho ya Bongo Opera yatakayofanywa na Lumumba Theatre Group .
Mmoja wa Waigizaji  Mammito Eunice Njokii kutoka nchini Kenya akizungumza kuhusu Igizo ambalo litaonekana katika maonesho ya Bongo Opera
Wageni waalikwa na wasanii mbalimbali wakifuatilia majadiloano mbalimbali yakiendelea wakati wadau wakizungumzia maigizo ya Bongo Opera
 Baadhi ya wadau wa sanaa ya maigizo wakizungumza.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...