Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
UJENZI wa daraja jipya la WAMI ,linatarajia kukamilika na kutumika Novemba mwaka 2022 ambapo kwasasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia  61.4.

Akitembelea na kupata taarifa ya Ujenzi wa daraja hilo ,Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi ,Pro.Makame Mbarawa amemuagiza Mkandarasi Power Construction Corporation Ltd kutoka China, kufanya kazi kwa masaa 24 kuanzia sasa ili ujenzi ukamilike haraka .

Waziri huyo ,alifafanua ujenzi unatarajiwa kugharimu bilioni 72 ,na upo kwenye hatua nzuri ya kuridhisha .

Alisema ,changamoto ya uchelewaji wa kufika vifaa kinyume na mpango kazi kutokana na uchelewaji wa meli kufikisha vifaa hivyo kutoka nje ya nchi kwa tatizo la Uviko 19 ilisababisha kuchelewesha mradi hivyo ifidiwe ikiwezekana mradi ukamilike hata Juni 2022.

Hata hivyo, Mbarawa alieleza ,daraja la WAMI la zamani lilijengwa 1959 na ni kiungo kutoka Chalinze kwenda mikoa ya Kaskazini mwa nchi yetu na nchi jirani .

"Daraja hilo halikidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa kuwa lilijengwa miaka mingi iliyopita na ni jembamba lenye njia moja, barabara zinazounganisha daraja hili ziko kwenye miinuko mikali na kona mbaya ambapo ajali mbaya na vifo vimekuwa vikitokea mara kwa mara ,"

"Hili jipya likikamilika litakuwa kubwa urefu wa mita 510 na upana wa mita 11.85 linajengwa umbali wa mita 670 pembeni mwa daraja la zamani ."alisema Mbarawa.

Mbarawa alieleza ,daraja hili litakuwa na uwezo mkubwa katika usafirishaji na kufungua milango ya kimaendeleo na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Awali akitoa taarifa ya mradi ,meneja wa TANROADS Pwani ,Andrea Kasamwa ,alisema mradi umefikia asilimia 61.4 ,muda wa mradi uliopita hadi sasa ni miezi 35.

"Hadi Sasa Mkandarasi amelipwa asilimia 15 ya malipo ya awali kiasi cha sh .bilioni 10.17 kulingana na matakwa ya kimkataba na ameshawasilisha hati tisa za malipo ya kazi alizofanya sh.bilioni 21.405 na kulipwa bilioni 18.399 ."

Kasamwa alibainisha ,kati ya hizo fedha sawa na asilimia 27 ya gharama ya mradi bilioni 67.779 .

Alieleza , Mkandarasi alianza kazi ya Ujenzi 22,octoba 2018 na kutakiwa kukamilisha mradi September 2021 miezi 35 lakini Mkandarasi amewasilisha sababu za kimkataba nyongeza ya muda wa ujenzi kufika Novemba 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...